Saturday, September 13, 2008

KISWAHILI

Mara nyingi huwa nakasirishwa kuona / kusikia watu wanatumia vibaya baadhi ya maneno ya kiswahili. Hapa nimechukua au nataka kutoa mfano haya maneno matatu. Karibu, Jambo na Habari

Karibu: Ni kuto kuwa mbali kwa wakati au mahali, kiasi cha kukadria. Lakini watu wengi wanaelewa zaidi karibu ni tamko litumikalo kuitikia hodi au wakati mtu anapokaribishwa au kupokewa mahali fulani.

Jambo: Watalii wengi wanafikiri wanaweza kiswahili, kusalimia wasemapo jambo hawajui kwamba Kiswahili sananifu hutamkwa hujambo/haujambo/hamjambo? kwani ukisema hivi anashindwa kuitikia sijambo. S afadhali hata wangefundishwa kusema hali yako.....

Habari: Neno habari limekuwa linanitatanisha sana. Kama kawaida maneno mengi ya kiswahili yana maana mbili azu zaidi. (1) Habari ni melezo ya jambo fulani lililotokea, taarifa, ujumbe na ripoti.
2) Habari hutumika katika kuamkiana na kuulizana hali. Lakini inaonekena wengi hatuwazi sana tunapoongea hili neno litumikeje.

2 comments:

Unknown said...

Nilikuwa sijui kumbe dadangu ni mwalimu wa Kiswahili, unajua watanzania (mimi mojawapo) Kiswahili inasumbua sana.

Hongera sana kwa somo.
Vipi unafundisha kiswahili kwa waswidi au?

Yasinta Ngonyani said...

hapana mimi si mwalimu wa kiswahli bahati mbaya. Ila ningependa. halafu unajua napenda sana kujifunza lugha. Sio najisifu lakini naweza kusema ninakipaji hicho.