Saturday, September 20, 2008

MAISHA MAGUMU NA MARADHI

Maradhi ya kuambukiza yanayompata mama mwenye mimba yanaweza kusababisha athari kwa mtoto anayezaliwa. Kama mama mwenye mimba atakuwa na kaswende, ataweza kuzaa mtoto kipofu, kiziwi, mwenye kifafa au taahira.
Mtoto akipokelewa vizuri katka ulimwengu huu, kama vile mama huyu anavyofanya kwa mtoto wake, inamfanya mtoto awe na matumaini na kuvumilia matatizo ya maisha katika utu uzima.

Mtoto huyu ana njaa na ametekelezwa. Hana mtu anayemsimamia haki zake za msingi (chakuli, malazi, upendo, elimu na malezi)
Mtoto kama huyu amekwishawekewa msingi mbaya wa maisha na ana hatari ya kuathirika kisaikolojia siku zote za maisha yake.

2 comments:

Anonymous said...

Pole sana mtoto maana hana kitu wala mtu. Lakini kuna watu wana chakula na sehemu ya kutosha pia uwezo wa kumtunza mtoto kama huyo. Pia kuna watu kila siku wanatupa chakula pia nguo chukua nafasi na saidia watu kama mtoto huyo.

Anonymous said...

mmmmmmmmm huyu anayenyonyesha ni wewe au nimekosea dadangu maana unamuangalia mtoto mpaka analegea shingo ha ha ha ha aha