Thursday, September 25, 2008

NALIPENDA JINA LANGU YASINTA

Mwenzenu leo nimepatwa na kichaa au sijui nisemeje : Yasinta ni jina langu, nataka kuwaambia ya kwamba jina Yasinta nalipenda sana. Nalipenda jina langu halafu napenda sana watu wanaponiita Yasinta napenda sanaaaaa. Napata shida kidogo ninapokuwa Tanzania wote wanasema Mama fulani au Nangonyani kiasi kwamba nasahau naitwa nani. Ila hapa Sweden wote wananiita jina langu lakini wananiudhi wanatamka vibaya wanatamka na H. Hyasinta. oooh wananiudhi sanaaaaaaa. Ila wao waninijibu ni kwamba wanaposema Hyasinta wanawaza au moja ya ua ambalo linaitwa Hyacint huwa linapatikana sana hapa wakati wa Noel.
Ni hili ua liitwalo Hyacint


Kila mara nawaambia Jina langu YASINTA si Hyasinta. kwa mara nyingine nalipenda sana jina langu. Asante baba na mama. Yasinta

5 comments:

Christian Bwaya said...

Kuna rafiki yangu moja anaitwa Yasinta. Ila yeye huandika Hyasinta. Any difference? Mimi nilidhani maana yake ni ile ile!

Una jina zuri sana dada. Hongera. Jivunie jian la Kiafrika.

Nimefurahi kutembelea blogu yako.

Anonymous said...

Hyasinya?????? siyo sahih kwani matumizi ya lugha yangongana kabisa. ila kiswahili na mengineyo ni Yasinta hta ikiwa kikoloni sawa. unajua wabongo wanapenda mambo au kufanya mambo pasipo kujihoji maana halisi. nakubaliana na dadangu Yasinta ndiyo sahihi kabisa wasiotaka wajinyonge

Christian Bwaya said...

@Anon hapo juu: Nimekuelewa. Nadhani kuanza na 'H' ni kukosea. Ladha ya jina zuri kama hili inapotezwa kabisa.

Ni sawa na kusema eti na mimi nianze leo kujiandika Bwayah, au Buayah.

Nampongeza Yasinta kwa kuliandika kwa silabi za kiswahili sanifu.

Unknown said...

Nani nalipenda Sana jina langu Yasinta

Anonymous said...

Yasinta forever