Monday, September 15, 2008

UNGEKUWA WEWE UNGEFANYEJE?

Umekuwa kijana/msichana wa umri wa kuoa/kuolewa. Umefunga ndoa na matunda yanaonekana. Watoto hao.
Lakini katika historia/ukoo wako wewe ni mtoto pekee kwa baba na mama yako.

Na wewe sasa una mume, watoto na kazi. Watoto wanaenda chekechea, mume ana kazi pia. Na wewe kazi yako mara nyingi mchana na usiku.
Mchana sio kitu watoto watakuwa chekechea au shuleni. Tatizo usiku, umejaribu kumwomba mama yako mzazi msaada awatunze wajukuu. Wajukuu ambao ndio hao tu ambao anao. Lakini kila mara anakataa. Je? ungekuwa wewe ungefanyeje?

2 comments:

Anonymous said...

Ningekuwa mimi kwa kweli ningekaa chini na mwenzangu (mume au mke) then tuangalie tufanyeje kwa mustakhabali wa watoto au mtoto wetu.
Kuhusu mama mkwe au baba mkwe kukataa wajukuu kwa upande wangu naona yupo sahihi kwani wakati mnazaa au ninazaa tulikubaliana kwamba watoto wangu atanitunzia? unapozaa watoto au mtoto ni jukumu lako mzazi kujua utamlea vipi. Kama mama mkwe anasaidia hii ina maana kwamba ni huruma yake tu ila halazimiki kuwatunza wajukuu zake ingawa hili linaweza kuwa ni suala la kiutamaduni zaidi kuliko wajibu, jamii nyingi za kiafrika ukiwa wa kwanza katika familia unapewa jukumu hata la kusomesha wadogo zako na pia wanaweza kuishi kwako wanavyotaka wao ila jamii zingine ni kama hawana huruma kila mtu na mzigo wake.
Ila huyo mamamke naona mgumu sana hata ile huruma hana ingawa kweli watoto ni wako na kutunza ni wajibu wako naona yeye kazidisha ingawa ana haki.
Hapo ni kusugua ubongo wazazi wenyewe kujua mfanye nini kwa watoto wenu. Mama mkwe ana hiari hawezi kulazimishwa na ana haki.
Mawazo yangu tu!

Lazarus 2nyi

Yasinta Ngonyani said...

Ni mawazo mazuri lakini kweli inawezekana bibi asiwe na upendo kwa wajukuu wake hata masaa matatu au angalao saa moja. Kama ulivyosema ana roho ngumu kama sio hivyo basi ana akili maalumu. na hii si story to ni kweli.