Tuesday, April 7, 2009

KUTHUBUTU KUONYESHA MAPENZI/UPENDO=MAISHA


Kuthubutu kuonyesha upendo wako,
sio tu maneno mazuri,
Na sio tu upendo wa matendo
Au maua na chaklet.

Ni kuonyeshana heshima,uaminifu na imani.
Kuonyesha wepesi wa kuona huruma wakati mwanzako anapokuwa na msongo/matatizo.
Kuwa msaidizi mwema na mwenye kusema ukweli.

Kuthubutu kuonyesha masikitiko yako,
Sio kila wakati kujifanya mwenye nguvu(mvumilivu),
Tukae/kaeni pamoja, tuthubutu kuwa watoto ndani yetu.

Tuwe sisi(Kuweni ninyi) kwa dakika chache,
Tuwe na dakika chache za furaha,
Tuwe na dakika cchache za huzuni
Tufante siku iwe ya shangwe.

Tushirikiane katika raha na taabu katika maisha,
Tuwe waaminifu, tukaribiane na tupeane joto.

11 comments:

Simon Kitururu said...

Hapo umemaliza dada!

Bennet said...

Mapenzi ni kujitoa kwa mwenzio
Mapenzi ni kushirikiana kimawazo na kimatendo
Mapenzi si karaha bali
Mapenzi ni kupeana raha
Mapenzi yataka usiwe mvivu bali
Mapenzi yahitaji uvumilivu

Fadhy Mtanga said...

Yap!
Mapenzi ni kuheshimiana, kuridhiana, kusikilizana, kujaliana, kufanyiana kila lililo jema. Kusaidiana.
Kulindana.
Ila umesema kuwa wakweli.
Ukimpenda mtu kwa dhati, nafsi inakukataza kumdanganya.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

eti heshima,uaminifu ndio nini? siijui misamiatai hii.

kwenye mapenzi naweza kuwa mwnafunzi kama ndo inabidi yawe hivi. nahitaji somo zaidi ili niyaweze. labda unielimishe yasinta

Mbele said...

Mimi nilikulia kijijini, na hisia zangu kwa kiasi kikubwa ni za mtu wa kijijini. Kule kijijini, wapendanao hawapaswi kujionyesha hadharani kama hiyo picha inavyoonyesha. Ni masuala ya faragha. Ndio mila za babu na bibi zetu. Nahisi hao vijana katika picha wameiga ya wazungu. Ila mimi ninaridhika na mambo yangu ya kijijini.

Koero Mkundi said...

Prof. Mbele kila kitu siku hizi tunawaiga wazungu!

Nuru Shabani said...

Aliyosema Prof,yanukweli ndani yake.
Yaani tunaiga hata namna ya kupenda!
Ndiyo maana wapenzi wengi huachana siku hizi kwa sababu ya kuiga.

Kibunango said...

Kuna utamu wake wa kuonyesha mapenzi hadharani...!

Anonymous said...

Prof. Mbele umepatia! mimi pia nimekulia kijijini na hata mapenzi yangu ni kama ya mwanaijiji, siwezi kufanya kila jambo mbele za watu, mapenzi ni faragha. na nashukuru nimepata mke mwanakijiji nae. wengi huwa wanaiga kila kitu, wengine hudai kufanya hivyo ni kwenda na wakati, swali wakati upi huo? wengine hudai kwa kufanya hivyo ni kuonyesha kwamba ni wasomi, wao ni tofauti na watu wa kijijini! kazi kweli kweli! nashukuru Mungu nimepata mwenzangu msomi na mwenye hisia na makuzi ya kijijini.

Yasinta Ngonyani said...

Yah, Nami na kubalia na baadhi ya watoa maoni ni kwamba haya mambo ya mapenzi kuonyeshwa wazi hivi si tamaduni kwetu hasi sisi tutakao kijijini. Huwezi kumkuta /wakuta watu wanashikana mikono, kupeana mabusu,kukumbatiana hadharani hakuna.

Na pia nakubalia kuwa maisha yetu ya sasa yamekuwa ya kuiga kila kitu. naona karibu tutaanza pia kuiga kula vyakula yaani kuuacha ugali na kisamvu.

MARKUS MPANGALA said...

Prof Mbele umemaliza kila kitu, wala sihitaji mwanamke wa kumpenda kumwonyesha mbele za watu nampenda. nahitaji mapenzi ya mimi na wewe faraghani wala hatuhitaji kuiga tu.

Koero hatuigi wote ila wewe labda unaiga, au nawe unavaa mawigi yale yanayouzwa toka ughaibu yenye fangasi????? ha ha ha ha ha ha ha hs poleeeeeeeeeeee mwanawane