Friday, April 24, 2009

BINADAMU KATIKA MAISHA YA ULAFI NA ULEVI


maneno ”mlafi” na ”mlevi”:- Walafi na walevi wapo, au tuseme tupo. Walafi wapo majumbani mwetu na huonekana pia kwenye sherehe ama sikukuu. Huonekana kwenye mazishi kunakotolewa chakula, nyama na pombe, huonekana kwenye matanga, maulidi na kadhalika. Si haba wanaokula kwa pupa na kupita kiasi wali, pilau, nyama, mikate, maandazi na matunda mbalimbali hasa ndizi, machungwa, embe na mapapai.

Wakati wa vyakula vipya au mavuno mapya, kesi za kuvimbiwa hujitokeza. Vyakula hata kwa kuvimbisha watu ni pamoja na maboga, matikiti na mahindi mabichi. Wengine huvimbiwa hata kufikia hatua ya kulazwa hospitalini ama kuchunguliaa kaburi kabisa. Walafi wengine walio wakristo hifikia umahututi hata wa kusaabisha kupewa hata sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa. Aibu kweli.!

Walevi nao ni wengi hapa duniani. Hata kama wapo walevi wa kujisifu kwa maneno tu, wapo wanofanya kweli. Hao wanaweza kuzikata pombe na vileo vya aina mbalimbali. Wao wanaweza kutembea pote. Wanaweza kubugia pombe yoyote iliyo karibu yao tangu ulanzi karanga, myakaya, wanzuki, chibuku hadi bia. Nazo bia ni aina zote, tangu Kilimanjaro, Ndovu, Tusker, Serengeti, Castle, Safari hadi Bingwa. Na katika uwanja wa pombe kali wamo pia. Wanaweza kuikata tangu konyagi, gongo hadi ”whisky” kali kama John walker na Vodka na zaidi.

7 comments:

Mwanasosholojia said...

Nimeipenda hii ya walevi dada Yasinta, imenikumbusha huu utafiti kuhusu pombe na walevi niliowahi kuukuta sehemu;
1. Pombe za Chimpumu, Dengerua, Kabungusi, Kangara, Komoni, Mbege na Chibuku- Hupoteza uwezo wa kufikiri wa mtumiaji.
Huongeza ufanisi wa viungo vya mwili vilivyo katikati ya miguu ya mtumiaji chini ya kiuno kwa mbele, hivyo kuongeza uwezekano wa mtumiaji kujiusisha na ngono zisizo salama na kubaka. Zaidi ya 60% ya kesi zote za kubaka zilizotokana na ulevi zimehusishwa na utumiaji wa pombe hizi! Pia,
Hukakamaza misuli ya midomo na kuongeza ufanisi wa koromeo (voicebox),hivyo si ajabu kuwakuta watumiaji wa pombe hizi wakipayuka ovyo na kwa sauti za juu kuliko kawaida.

2. Pombe za Pingu na Gongo
Hupunguza kwa kiasi kikubwa uwezo wa kufikiri wa mtumiaji
Huongeza joto la mwili la mtumiaji kwa kuongeza spidi ya metabolism(metabolic activities), hivyo kuongeza uwezekano wa mtumiaji kuvua nguo hadharani, ili kupunguza joto la mwili!
Kwa upande wa pombe ya pingu, hii huongeza spidi ya myeyusho wa chakula(Digestion) na ikitokea mtumiaji hajala kwa muda mrefu huishia kutapika mpaka nyongo. Baada ya kuongeza spidi ya myeyusho wa chakula pombe hii hulegeza vifuniko vya mwili (sphincter muscles) hivyo kuongeza uwezekano wa mtumiaji kuachia kokoo madimba iliyo rojorojo(uharo wa nguvu na wenye harufu kali).Msicheke jamani...ni kweli hii!
Kwa watumiaji wa lile gongo litengenezwalo kwa kinyesi cha binadamu(kigamboni ni eneo maarufu kwa biashara hii), wengi wao huishia Intensive Care Units(ICU), na baada ya hapo hupelekwa Psychiatric Units(wodi za vichaa), kwani zaidi ya 63% ya watumiaji wa pombe hii huishia kuwa vichaa kamili!

3. Pombe ya Mnazi
Kiasi cha ulevi (alcoholic contents) kilichomo katika pombe hii,hushambulia sehemu ya ubongo wa kati (cerebellum), ihusikayo na kutunza utashi, hivyo si ajabu kwa mtumiaji wa pombe hii kuishia kuvurumusha matusi ovyo na kuyumba barabara nzima!
Iwapo mtumiaji wa pombe hii hatakuwa mwangalifu na hivyo kunywa mdudu fulani aitwaye kigoto anayekuwa katika pombe hii, basi mtumiaji huyo atakuwa mlevi mbwa wa mnazi maishani mwake!
Watu hushauriwa kuviepuka vyoo vilivyotumiwa na walevi wa pombe hii kwani harufu wanayoiacha huko chooni inahusishwa na kuongezeka kwa magonjwa ya saratani ya pua na ubongo (nose and cerebral cancer)

4. Pombe ya Ulanzi (Watu wa Mahenge Ulanga, Morogoro na Iringa, sijui kuna kaukweli kokote?...)
Pombe hii hushambulia viunganishi vya mwili (Body Joints), kwa hiyo asilimia kubwa ya watumiaji wa pombe hii huishia kulala mabarabarani,vyooni na sehemu nyingine zisizo za kawaida kwa kushindwa kutembea!

5. Pombe za Bia, Konyagi, Wiski, Gin na Wine mbalimbali (Hapa sasa jamani mi ngoja ninyamaze tu..nachelea ugomvi na waheshimiwa...) ila utafiti unaonesha kuwa....
Pombe hizi huongeza hali ya kujiamini kwa watumiaji na pia kuwakumbusha kuwa hapo zamani za kale, waliwahi kupitia shule,hivyo si ajabu kuwakuta watumiaji wa pombe hizi wakizoza kimombo na kujihusisha na mijadala isiyo na kichwa wala miguu punde baada ya kulewa! Hali kadhalika, kama ilivyo kwa Chimpumu, Dengerua, Kabungusi, Kangara, Komoni, Mbege na Chibuku, Pombe hizi hushambulia sehemu zilizo katikati ya miguu chini ya kitovu kwa mbele ya mtumiaji na kuzifanya sehemu hizo kuwa imara na zenye nguvu(strong and active) na hivyo kuongeza uwezekano wa kujihusisha na ngono zisizotarajiwa na zisizo salama!

Bennet said...

Huyu mzee kwenye picha lazima atakuwa testa, yaani pombe haiuzwi kijijini mpaka aionje yeye na kuipitisha ndio wengine waanze kunywa

Kibunango said...

Kuna wanywaji wa Pombe na walevi wa Pombe... Binafsi sijakufahamu unalenga wapi katika tundiko hili?

Anonymous said...

Du mzee anapata uchwara maridadi kabisa. Mkuu mwanasosholojia umenikumbusha misemo ya kisasa "ngono zisizo salama", maana siku hizi majukwaani ni nadra sana ukasikia habari za uzinzi. Siku hizi uzinzi umepata jina mbadala au ngono zembe aka zisizo salama au ngono salama! kazi kweli kweli!!

Mwanasosholojia said...

Teh Anonymous (April 26, 2009 12:15 AM)hizo sasa ndio sarakasi za utandawazi katika matumizi ya maneno. Ni kama vile tu ambavyo wakoloni siku hizi tunawaita washirika katika maendeleo (partners in development). Teh!

John Mwaipopo said...

Kwanza nilidhani mie mlevi kumbe aah wapi (kulingana na maelezo yako ya mlevi). mie ni mnywaji wa kawaida ila wa kila siku, isipokuwa nikiwa mgonjwa.

Kilichonigusa sana ni hiyo picha. Yasinta kweli una mambo! Sijui emeitoa wapi hii. Kwanza inaonyesha pombe 'imeiva'. Pili huyo mzee ama hajawahi kuiona bia, ama kama keshaiona hana shida wala kisebusebu nayo. Tatu imenikumbusha mbali sana. Najua mmeshaelewa! Taste buds zangu zinapata shida sasa.

alamsiki

Anonymous said...

PICHA iliyotumika Ni mfano tu.

Yumkini mzee huyo siyo mlevi wa kupindukia.
.....ona alivyo msafi na hajalewa bado.
Ni ama anatest au anakunywa mbege taratibu kwa kupokezana na wenzake.