Saturday, November 7, 2009

MAISHA NI KURIDHIKA NA ULICHONACHO!!!!

Hapa ni mimi na mume wangu wakati ni kikongwe!

Sio lazima kuendesha Mercedes, Land Rove, X6 au Hummaer ili kujiona wa maana. Watu wenye furaha sio muhimu kuwa na kila kitu kizuri. Tufurahie kile (kitu )tulichonacho.
!!!!!!!!JUMAMOSI NJEMA JAMANI!!!!!

9 comments:

Chacha o'Wambura said...

Kwa wengine maisha ni vitu na hapo ndo nongwa inapoanzia...lol

tunashindwa kuwa sisi...bahati yako Yasinta wewe ni wewe...lol

Ridhiko la kweli linatoka wapi?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

moyoni @chacha

Fadhy Mtanga said...

Vitu vinapaswa kutumiwa na watu kupendwa, hapo twaweza ridhika.
Lakini dunia ya leo, vitu vyapendwa na watu wanatumiwa, ridhiko haliwezi kuwapo.

Mdoti com-kom said...

Yasinta umesema kweli. Ipo hali ya watu kutokuw determined and being pushed by others. Anataka kuwa kama fulan bila kujua fulan kawezaje kuwa vile alivyo. Bila kuwa malengo yanayolingana na uwezo wako unaishia kupata msongo wa mawazo. "Karibu kwenye kibaraza changu kipya"

chib said...

akina dada wengi huwa ndio wanakuwa na fyongo!! Ukileta bike mh.... Furahia jumamosi yako

Unknown said...

DADA MIE SISEMI.....

Bennet said...

Wengi hatuna mioyo ya kuridhika na tulicho nacho, na huwa na tamaa ya kuwa kama wengine na hata ikibidi kuwazidi
Kwanza inabidi kujikubali mwenyewe kisha utambue kwa wao ni tofauti na wewe

Simon Kitururu said...

Tukumbuke kitu kizuri ni jinsi tu mtu afikiriavyo na ndio maana katika vitu vyote duniani vijulikanavyo vipo , bado kuna wapendao vikojoleo.:-(

Yasinta Ngonyani said...

Ndio ChaCha mimi ni mimi. Na nashukuru kwa hili. Ridhiko la kweli ni moyo wako kama alivyo sema Kamala asante Kamala.

Fadhy lakini wewe ukisharidhika na ulicho nacho na jinsi ulivyo inatosha.

Mdoti com-kom kwanza karibu sana hapa kibarazani na asante kwa maoni yako.

Chib! kurika sio akina dada tu ni kwa wote.

Kaka Kaluse! kwa nini hutaki kusema?

Kaka Bennet! Nanukuu "Kwanza inabidi kujikubali mwenyewe kisha utambue kwa wao ni tofauti na wewe" mwisho wa kunukuu. Hapa umenena kakangu

Mtakatifu Simon! Nimekuelewa:-)