Wednesday, November 18, 2009

+RAFIKI YANGU MPENDWA AGNESTA MAPUNDA+

Kutokana na sheria au sijui niseme mipango ya Tanzania kuwahamisha/shwa walimu:- Nakumbuka ilikuwa mwaka 1985 baba alipata uhamisho kutoka Lundo s/m kwenda kijiji kimoja chenye shule iitwayo Kingoli. Nilikuwa darasa la tano. Nilipofika pale shuleni nilikutana na wanafunzi wengi, lakini Agnesta alinipokea kwa namna yake.
Tulianza urafiki wetu, uarafiki ambao tulikuwa wakati wa jumamosi au jumapili tukitembeleana majumbani. Yaani, tulikuwa tukitembeleana, huku tunachuklua zawadi(ndundu) unga kwenye jamanda na kuku. Na ukifika kwake unachinjiwa kuku pia.

Nliachana mwaka 1988 na rafiki yangu Agnesta. Mwaka 2007 nilikuwa nyumbani TZ. Siku moja nilikuwa mjini – Songea, katika pitapita ghafla mtu akanishika bega na kunisalimia dada Yasinta shikamoo! Nikashtuka na kugeuka alikuwa mdogo wake Agnesta. Nikasema moyoni AHSANTE Mungu. Kwa kufurahi kupata habari za rafiki yangu Agnesta. . Lakini habari nilizozipata hazikuwa nzuri Agnesta rafiki yangu alikuwa hayupo tena nami alishafariki muda mrefu labda miaka mitatu iliyopita. Sikuamini masikio yangu, nilisikitika sana , kwani alikuwa rafiki yangu mpendwa. Na leo naona amenishukia nkwani nimemkumbuka sana ndio maana kisa cha kuandika hapa. Mwenyezi Mungu Aiweke Roho yako PEPONI AMINA..

11 comments:

John Mwaipopo said...

such a sad nostalgia!

MARKUS MPANGALA said...

NAMANI NINGEMWONA,
ILI NIMJUUE VEMA,
NIMWAMBIE YA MAA,
YASINTA WA MAANA

LAKINI BAHATI SINA,
KAREJEA KWA KARIMA
AJUAYE YEYE MOLA,
SIKUYE IJAPOKUWA.

MUNGU AWE NAYE DAIMA

Mbele said...

Pole sana kwa kupotelewa na rafiki yako. Umeelezea vizuri kumbukumbu hii.

Vile vile, maelezo yako kuhusu mila ya wanawake kutembeleana wakiwa wamebeba "lijamanda" na kuku ndio mila ya kwetu Umatengo pia. Katika kitabu changu cha Matengo Folktales, ambacho ni mkusanyiko wa hadithi kumi za kiMatengo nilizorekodi miaka ya sabini na kitu na kuzitafsiri kwa kiIngereza, kuna hadithi moja kuhusu akina mama ambao wanatembeleana namna hiyo.

Katika maelezo yangu kuhusu hadithi hii, nimeongelea mila hii ya "lijamanda" na kuku. Habari yako imenikumbusha mbali. Shukrani.

Faith S Hilary said...

Mmh pole dada...yaani ukiwa na rafiki kama hivyo anakuwa so attached to you yaani u feel like u r sisters...RIP

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hongera kwa kumchagulia Mungu pahala pa kuiweka roho yake.

swali: kuna post uliitundika juu ya sijui wanaume kamaliza nini nini haraka sijui nini,, mbona siioni?

Halil Mnzava said...

Pole sana,
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.AMINA!

chib said...

Mimi nasema ndio MAISHA. kaza moyo na kusonga mbele

Unknown said...

pole sana dada, najua ni huzuni kwako kuondokewa na rafki yako mpenzi agnesta

upepo mwanana said...

Naomba niwe mgeni wako katika blogu hii

Anonymous said...

Yasinta, ledsen for din skull men sant ar livet... vi borde uppskatta vanskap dagligen...tack att du finns i mitt liv!

Yasinta Ngonyani said...

Napenda kuchukua nafasi hii na kuwashukuru wote kwa kunifariji kwani nimekuwa na mwazo mengi sana wiki hii. Naamini sisi ni familia moja ndio maana huwa tunafarijiana. NAWAPENDENI WOTE.