Tuesday, November 10, 2009

UJUMBE KUTOKA SWEDEN KWA KAKA LAURENT KINUNDA

Kaka Laurent Kinunda.
Katika ukuaji wangu/akili yangu nilikuwa nafikiri ya kwamba ndugu ni yule mliyezaliwa mama mmoja na baba mmoja. Lakini kumbe nilikuwa na mawazo finyu. Ndugu ni mtu yeyote yule sio TU yule mliozaliwa tumbo moja.

Ilikuwa mwaka 1993 nilipokutana kwa mara ya kwanza na kaka LAURENT KINUNDA. Kaka Laurent, napenda kukushukuru kwa moyo ulio nao, wema wako na upendo wako. Umekuwa karibu sana nasi. Umekuwa huna kinyongo na familia yangu mara kunapotokea shida pia kunapokuwa na raha unakuwa nasi.

Nakumbuka kila tujapo TZ, hakuna mwingine anayekuja kutulaki uwanja wa ndege, isipokuwa ni wewe kaka Kinunda. Kwa hili napenda kutoa shukrani zangu/zetu za dhati. Umekuwa nasi katika matukio mbalimbali na umetusaidia na unatusaidia mambo mengi ambayo siwezi kuyahesabu hapa. Ninachoweza kusema. NAOMBA MWENYEZI MUNGU AKULINDE WEWE NA FAMILIA YAKO MUWE NA AFYA NJEMA NA MAISHA MEMA. TUNAWAPENDA WOTE. UPENDO DAIMA.

11 comments:

viva afrika said...

mola atambariki na kumwongeza mara dufu, nawe kwa shukrani za dhati "ubarikiwe sana".

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

amen

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti said...

Mjukuu wako anasema hivi: 'ni watu wachache wanaoweza kukumbuka fadhila na kutoa shukrani'. hivo nawe twakushukuru kwa kuwa na moyo wa shukrani.

Biblia yasema 'ubariki nawe utabarikiwa' sikumbuki ni fungu la ngapi labda Mt saaaana Simon aweza kutukumbushia...lol

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti said...

Mjukuu wako anasema hivi: 'ni watu wachache wanaoweza kukumbuka fadhila na kutoa shukrani'. hivo nawe twakushukuru kwa kuwa na moyo wa shukrani.

Biblia yasema 'ubariki nawe utabarikiwa' sikumbuki ni fungu la ngapi labda Mt saaaana Simon aweza kutukumbushia...lol

twenty 4 seven said...

mora ambariki...

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kama alivyosema "Ng'wanambiti" - ni watu wachache wakumbukao fadhila walizotendewa. Wengi husahau fadhila mapema na kuanza kulalamika na kulaumu unapowasitishia misaada. Asante kwa moyo huu.

Chacha - mbona unajiita Ng'wanambiti?

John Mwaipopo said...

blessed is the hand that giveth, not the one that taketh.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti said...

Matondo, hilo ni jina nililopewa wakati nakwenda kwenye ngoma za 'manyalali'...lol

PASSION4FASHION.TZ said...

Na kweli sio wote wanakumbuka fadhila,na wewe ni wapekee ubarikiwe sana.

Mbele said...

Dada Yasinta, naungana na wadau wanaosema unafanya vizuri kukumbuka fadhila. Halafu, hao akina Kinunda asili yao ni kwetu Litembo, kule juu milimani Umatengoni. Basi leo umenifanya nitembee kifua kijuu :-)

Yasinta Ngonyani said...

Nachukua nafasi hii kwa kuwashukuru wote kwa kumsalimia kakangu wa hiari. Kaka Kinunda Ubarikiwe sana na Mungu na uendelee kuwa na Moyo huo huo ulio nao ikibidi zidisha. Sisi hatutakusahau milele.