Wednesday, July 21, 2010

Mlevi anapolewa chakari na kuanza kuongea!!!!

"Mlevi anapolewa chakari na kuanza kuongea unapaswa kumsikiliza kwani wengi wao huongea yale yaliyoko mioyoni mwao. Uhusiano wa pombe na ufanyaji kazi wa ubongo husababisha mlevi kunena yale yaliyoko moyoni mwake bila ya simile"- Mwalimu Malekela, Tabora Boys 1994.
Swali ni kwamba, je utafaidikaje na uvumbuzi huu? Nadhani ni kwa kuchagua yale yatokayo kwenye kinywa cha mlevi kwani si yote yatakuwa ni yenye kujenga. Mengi yatokayo kwenye kinywa cha mlevi hutokana na migogoro iliyoko ndani ya mioyo yao. Mara nyingi migogoro hii inakuwa ni ile isubiriyo suluhisho.
Katika jamii yangu mara nyingi nimeshuhudia tabia ya baadhi ya watu pale inapotokea kutokuelewana na wenzao, basi huenda kunywa pombe na kisha kurejea kwa mabishano zaidi. Je kuhusu wale wanaume wanaopenda kupiga wake zao pindi wanapolewa? Je hii nayo inasababishwa na migogoro au inakuwa ni tabia ya kuzoea? Au pale daktari au mwalimu anapohitaji glasi mbili au tatu ili waweze kufanya kazi zao? Hii inakuwaje?? Je kuna uhusiano kati ya unywaji pombe na ufanisi katika kazi? Je umepata kusikia kuhusu yule daktari bingwa wa upasuaji ambaye ni lazima apate kinywaji kwanza ili aweze kutenda kazi yake vema?
Habari hii nimetumiwa na msomaji wa blog ya Masha na Mafanikio na kuniomba niiweka hapa kibarazani ili tujadili kwa pamoja. Haya wapendwa karibuni na tujadili. Umoja ni nguvu .....

12 comments:

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Hiyo kali kuliko gongo!

Yawezekana ni kweli kwani mlevi akikupa lake ni la nguvu.

Lakini nashangaa kwa nini mtu anaweza kushindwa kukwambia jambo akasema ngoja nikakunywee kidogo!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mmh pombe inapunguza aibu ya kutaka kusema pumba zako, sijui

ila ulevi una negative effects kuliko positive ones

Unknown said...

Kama alivyosema kaka Kamala, pombe inafyatua fyuzi ya aibu na kukufanya unene bila ya simile. Ndipo hapo basi tunapopata kusikia yale yenye busara pamoja na pumba kama zikiwepo. Cha msingi ni kusikiliza kwa makini na kuchagua lile lililo jema. Ahsante kwa mada tamu...

Unknown said...

Swali la kizushi... inakuwaje kuhusu chizi??? Akiwa mitaani ananena naye asikilizwe? Pande spesho kwa kaka Kamala, naomba jibu!

Anonymous said...

lakini mara nyingi walevi wakiamka hasubuhi hawana kinyongo tena

Marefu said...

Habari hii ya walevi inanikumbusha wakati nasoma somo la acting bale university of Dar es Salaam. Mwalimu wangu alikuwa anapenda sana kutumia mhusika mkuu kama "mlevi". Na huyu mlevi alikuwa ndio muongeaji mkuu wa zile point zote muhimu kwenye mchezo. Hivyo basi ninaungana na mtoa hoja kuwa mlevi huwa anaongea yale yaliyo moyoni mwake, siyo mtu wa kumbeza.

emu-three said...

Mtu akilewa huwa mlevi, na anachokifanya kinaweza kikawa nje ya matakwa yake, sidhani kama kweli inaweza kuwa zile fikira zake ambazo zipo moyoni. Inaweza ikawa baadhi ya fikira zake, mafano mtu kujikojolea, kutukana au kupiga wenzake na hata kumtukana mzazi wake, haya inawezekana alikusudia awali. Hapana nafikiri kutokana na kulewa , ile akili ya kawaida ambayo mtu anakuwa nayo ya kujizua usifanye yale yasiyotakiwa inakuwa haina nguvu. Kwa namana hiyo kila linalokujia linakuwa halichijwi linakwenda moja kwa maoja katika kulitenda.
Mlevi wakati mwingine hana tofauti na mwenye upungufu wa akili, kwani wote wanafanya matendo yanayofanana. Kwasababu hakuna mchujo wa matwaka ya akili, nifanye hiki au nisikifanye kwa sababu kadhaa...
Naona ndio yangu kwa leo
emu-three

Penina Simon said...

Duh!! hapo nilitamani ningepata ni kwanini wengine hulewa nakuamua kutandika wake zao,badala ya kutandika walevi wenzao waliokuwa wakilewa nao, pia nilitamani kusikia kuhusu huyo Dr. manake nilishawahi kusikia Dr. shaba, akisema kuwa ili aweze kuingia muchuari na kufanya upasuaji kwa maiti ni lazima apige kinywaji kimkolee, je pombe inahusiana kuwa jasiri? au inafuatana na akili ya mtu au wanafuatia ule usemi wa kunuiza unapokusudia kuwa kile kilevi kikuwezeshe kuwa vile unuizavyo, sababu naona watu wengine wakinywa pombe huwa mazoba (watahira/wajinga wajinga). Unaweza nisaidia kamauna majibu ya hayo?

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Penina: huyo daktari amesomea Urusi?

Manake wanasema walosomea urusi ndo vodka kwao ni kama juice/desert asubuhi, muchana na jioni kama dozi ya panadol...lol!

John Mwaipopo said...

mnazunguka nini si mniulize mimi tu.

Blackmannen said...

Mtu anapokuwa anakunywa anapitia stage 4 za hali ya kufanya kazi akili yake na mwili kwa ujumla. Kutegemea na aina ya kinywaji anachokunywa.

1.Anapoanza kunywa glasi au chupa (kama ni beer) ya kwanza hujisikia kuchangamka. Anaanza kuongea maneno mengi ya busara na anasikiliza wakisemacho wengine kwa makini.

2.Anapoendelea kunywa, ndipo pale anapoanza kuongea kwa sauti ya juu na kutokuwa na subira ya kusikiliza wengine kuongea.

3.Anapoendelea kunywa "resistance" ya mwili pamoja na akili hupungua, na hapo ndipo anapoanza kujiona anaweza kila kitu. Ukimpinga anachosema anaweza kukupiga, anajisikia ana nguvu kuliko mtu mwingine.

Aibu humtoka akilini mwake. Hapo ndipo anapofanya madudu yote ya aibu bila uoga hata kumpiga mkewe.

4.Anapoendelea kunywa au kuendelea kukaa katika chumba chenye watu wengi na hewa kidogo, hapo ndipo hulewa zaidi. Pombe hupanda kichwani.

Atanyamaza kuongea na kuanza kusinzia. Baadaye ataanza kuona kizunguzungu na kujisikia kutapika. Mwili wake huanza kukosa mawasiliano.

Akitapika hupoteza kumbukumbu, anaweza kujikojolea na mwili wake wote unakata mawasiliano kabisa, hata kama atajiumiza hatasikia maumivu. Akilala hulala fofofoo. Huyo ndiyo "Mlevi".

It's Great To Be Black=Blackmannen

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@mrope, unatambuaje kama huyu ni chizi na huyu sio?? uchizi una definition yake. hata wewe au mimi kuna baadhi ya wakuonao ni chzi japo wewe sio.

kwa hiyo uamuzi ni wako lakini kumbuka machizi wengi huwa na point pia au wanafurahisha