Monday, July 19, 2010

Siamini kama wewe ndiye yule kabla hatujaoana!

Je sijakuwa makini??
Inawezekana baada ya kuishi katika mahusiano ya uchumba sasa umeoa au kuolewa, Karibu sana kwenye chama kubwa, chama la ndoa, ulimwengu mpya kabisa, ambako mapenzi huchukua sura mpya ya uhalisia.

Sasa kila kile uliona si tatizo kwa mchumba wako unajikuta kinakuudhi, namna anavyotafuna chakula sasa inaudhi, namna anaweka muziki katika sauti ya juu sasa inaudhi, namna anaacha nywele kwenye sink bafuni sasa inaudhi, namna anaacha taulo lenye maji bila kulitundika ukutani inaudhi.

Namna anaacha kitanda bila kutandika inaudhi, namna anavyokoroma akilala usiku sasa inaudhi, namna anavyoacha drawer za makabati bila kuzifunga inaudhi sana, namna anavyoacha kuweka nguo na makoti kwenye hanger sasa inaudhi mno, namna anavyoongea bila break sasa inakuudhi sana, list inaendelea ..............................
Kumbuka wakati wa uchumba hivi vitu uliviona vidogo sana na kwamba hakuna tatizo!

Swali la kujiuliza je, nini kimetokea kwa ule upendo (fall in love)?
Ilikuwa ni illusions kukusababisha ujipeleke mwenyewe hadi kusaini mkataba wa ndoa na kukiri kwamba hadi kifo, katika raha na shida, katika afya na ugonjwa na inawezekana wewe ni mmoja ya wale ambao wanalaani sana ndoa walizonazo kwani wale ambao kwanza waliwaambia NAKUPENDA NA NITAKUPENDA wamewadanganya na sasa unajikuta upo kwenye ndoa ambayo kila siku hali ni mbaya.

Una haki ya kukasirika kwani ni kweli ulidanganywa na tatizo lilikuwa ulipokea information ambazo hazikuwa sahihi. Na hizo information zilikuwa ni ile hali ya kupendana (fall in love) ambayo katika ukweli si upendo wa kweli bali ni illusions.
Kale kakichaa ka kuamini kwamba tutapendana milele bila kuumizana wala kukwazana kangedumu na kuwa hivyo siku zote.
Katika asili “fall in love” ni mating character ya binadamu kuhakikisha mke na mume wanavutiana ili kuhakikisha species inaendelea (survival) na si upendo wa kweli.

Ulikuwa tayari kuacha kusoma kwa ajili ya mitihani ili kuwa na mpenzi wako maana yeye alikuwa muhimu mno.
Uliacha kwenda kwa rafiki zako hata ndugu zako kwa kuwa ulimpenda sana mchumba wako.
Uliacha hata kwenda kusoma au kwenda kazini ili kuhakikisha unampa mpenzi wako kile moyo wake unakipenda (to make her/him happy)

Kijana mmoja alikiri kwamba
“Tangu nimekutana na huyu binti, nimempenda, siwezi kufanya kitu chochote tena, siwezi kuwaza kuhusu kazi kwani kila wakati nawaza na kuota kuhusu yeye.
Hamu niliyonayo ni kumfanya yeye awe na furaha muda wote, nipo tayari kufanya jambo lolote kuhakikisha anakuwa na furaha”.
Yaani mtu akili inahama hadi unajiona wewe ni Mama Theresa kwa maana ya kutoa kila kitu ili kuonesha upendo kumbe ni illusions.

Kumdondokea mtu (fall in love) ni hali ambayo hudanganya na kumfanya mtu ajione kweli yupo katika upendo wa kweli. Huamini kwamba hakuna tatizo linaweza kuwepo kila kitu ni shwari.

Baada ya hali ya kudondokeana (in love) kuchuja (kawaida baada ya miaka 2) ndipo mtu huanza kurudi kwenye ulimwengu halisi.
Ndipo unaanza kugundua yale unayapenda na kuona kumbe ni tofauti na yeye anayoyapenda.
Unajikuta wewe unapenda sex na yeye anajisikia kuchoka na hapendi.
Unapenda kununua gari kwanza na yeye anapenda mjenge nyumba kwanza.
Unapenda kutembelea wazazi wako yeye anasema hapendi mtumie muda mwingi kwa wazazi wako.
Unapenda kwenda kuangalia match ya mpira wa miguu (soccer), anakwambia unapenda mpira kuliko yeye.

Kidogo kidogo ule moto wa mapenzi ya kwanza (fall in love) huanza kuyeyuka na kila mmoja sasa anaanza kujikita kwenye kujipenda yeye na mambo yake, kujihisi na kuwaza kivyake na sasa mnazidi kuwa watu wawili tofauti.
Bila kufahamu namna mapenzi yanapanda na kushuka mnaweza kuishi kuachana

Nimeipenda mada hii na kwa vile wote tuna lengo moja nimeona si vema kama nikiweka katika kibaraza hiki cha maisha na mafanikio zaidi gonga hapa. Haya karibuni tujadili kwa pamoja.

4 comments:

emuthree said...

Hii mi mada nzuri sana, na wengi huwa wanajadili kwa kuvutia upande wake, yaani waume kwao na wake kwao. Lakini watu tunasahau kuwa unapomnyoshea mwenzako kidole kimoja vitatu vinakuelekea wewe na kimoja kinaelekea juu kikisema ni mapenzi ya mungu, au tumuachie mungu, au tumetegemee yeye.
Wengi tunapoingia kwenye ndoa tunakuwa kama tumetosheka na kuitwa bwana na bibi na kusema tumefika lakini sidhani kama mkishaoana ndio mwisho way ale mapenzi ya kabla, nafikiri ndio mwanzao na sehemu hutu yakuonyeshana kila kitu. Chukulia mfano wa dakitari ukishapata udakitari au ualimu hawezi kuridhika na hicho cheo, lazima ataibobea taaluma yake zaidi na siku zinavyokwenda ndivyo anavyoongeza uzoefu, sasa kwanini ndoa iwe kinyume hapana unahitaji kujifunza zaidi unahitaji kuisomea ile kazi ili ujue zaidi na ili usisahau kile ulichojifunza. Sasa iweje ndoa, iweje mapenzi iweje upendo uwe hivyohivyo itakavyokuwa.
Nafikiri kuna makosa makubwa ya kutoijali hii hali ambayo ni nusu ya maisha. Inahitajika wati kabla ya kuoana waende shule, na sio lazima shule ya majengo, hapana, zamani kulikuwa na unyago na viti kama hivyo, kwasababu wazee wetu waliona mbali, sasa kuna elimu za mitandao, kuna elimu za vitabuni kuna elimu kwa kupitia akina shangazi, wahimizeni wanandoa kabla hawajaoana wapate mafunzo hayo!
Tujue ndoa ni nusu ya maisha yako, kwahiyo inahitaji sana virutubisho kama mbolea kwenye bustani, ili maua yaweze kuchanua. Na hivyo itawezekana kama vyema ndoa ni nini,masharti yake ni nini mapenzi nini na nifanyeje ili mapenzi yadumu(sio kuwekeana limbwata)yhaya mapenzi yana vina na mizani yake, Tukiyajua hayo kamwe mabadiliko hasi hayatatokea.
Kila mmoja ana nafasi yake katika kulifanikisha hilo, kwani kila mmoja anaweza kwa mahali pake. Haitakiwi kutegeana. Kwa mfano kuna jamaa mmoja alisema mapenzi ya wengine ni sawa na gogo. Lenyewe limelala linasubiri mchongaji au mwenye shida nalo alichonge anavyotaka. Haya ni makosa, mapenzi yanatakiwa yawe kama maji kubadilika kutegemeana na chombo sio kama gogo mpaka lipate mchongaji.
Nafikiri tukijitahidi kila mmoja kwa nafasi yake hata huo usemo wa `mbona wewe siye yule kabla hatujaoana utakuwa msamiati. Kwa kumalizia hebu isomeni makala yangu niliyoitoa kwenye blogi yangu, http://miram3.blogspot.com/2010/07/je-ndoa-ni-kaburi-la-mapenzi.html

Zaidi tuulizane
Emu-three

Upepo Mwanana said...

Yaani, mada hii imenigusa sana, nimeneemeka kwa somo.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Ungekuwa una ufahamu usingesema 'huyu ndo nilooa/olewa naye' ama nilokuwa nakula naye good time kabla hatujaoana!

Kwa hiyo: NI UJINGA KUSEMA HIVO!!!!!

Ni sawa na mtawa mmoja alonambia kuwa aliingia kwenye utawa kwa kuwa aliona maisha ya baba na mama yake hayakuwa yanamvutia. Nkamuuliza vipi kuhusu kuonjwa sasa? Akabaki kucheka tu!!!!!

Pole na kama ukitaka kuishi kwa raha yaone maisha kama sarakasi fulani ama igizo la ze komedi ambalo linakusaidia kujifunza maisha kwa mtizamo chanya saidi!!