Monday, May 30, 2011

BREAKINGNEWZZzz HALI SI SHWARI SEKONDARI YA TOSAMAGANGA IRINGA FFU WATUMIA MABOMU ..

Polisi wakiwaweka chini ya ulinzi wanafunzi eneo la Kitwiru nje kidogo ya na Manispaa ya ringa hapo ilikuwa ni kabla ya kuanza kupiga kurusha mabomu ya machozi.

Mwanakijiji kushoto akiwa na mwandishi wa habari wa Radio wa Ebony Fm wakifuta machozi kutokana na mabomu yaliyopigwa na askari na hao kuwatawanya wanafunzi hao.


Mwandishi wa habari wa Ebony FM akikimbia moshi wa mabomu ambayo yalikuwa yakipigwa na askari hao kutawanya wanafunzi hivi punde.


Wanafunzi wa Sekondari ya Tosamaganga wakikimbia moshi wa mabomu yaliyokuwa yakipigwa na polisi.


Hapa wakikimbia porini kunusuru afya zao chini ya vifaa vya wanafunzi vilivyotelekezwa


Hali ya usalama si shwari katika shule ya sekondari Tosamaganga wilaya ya Iringa mkoani Iringa hivi sasa wanafunzi zaidi ya 10000 wapo porini wakikimbizwa na polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia ambao wanatumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanafunzi hao ambao walikuwa katika maandamano ya amani kwenda ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa kuulalamikia uongozi wa shule hiyo.

Hadi hivi saa mabomu zaidi ya 10 ya machozi yamepigwa kuwatawanya wanafunzi hao ambao baadhi yao wanadaiwa kujeruhiwa kwa kuchomwa na miti wakati wakikimbia porini kukwepa mabomu hayo huku wananchi wa Mseke wakikimbia nyumba zao .

Polisi wamewazuia waandishi wa habari akiwemo mmiliki wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com ambao waliokuwepo eneo hilo wakifuatilia tukio hilo kuendelea kuchukua habari hiyo .
Picha na habari ni kwa hisani ya kaka Francis Godwin wa http://francisgodwin.blogspot.com/

4 comments:

Malkiory Matiya said...

Nalaani kwa moyo wangu wote vitendo vya polisi wa Tanzania kutumia mabavu badala kutumia elimu, ujuzi na maarifa ya kazi walizosomea. Laiti polisi wangekuwa wanaelewa jukumu lao la kulinda usalama wa raia na mali zao yote haya yasingetokea.

Raymond Mkandawile said...

hiyo ndiyo bongo yetu mambo tambalale kabisa.vyombp vya dora vinatumia madaraka yake kama vitakavyo bila kujali haki na ustawi wa wananchi wake.Vijana wanataka haki yao sasa kwa hali hiyo uongozi wa shule utaendelea kuboronga tu kwani wanapewa nguvu na dora.....Lakini swali langu ni kwamba hadi lini hali hii itaendelea?
Hadi lini haki za wanyonge zitaendelea kuchukuliwa na wenye nguvu wachache?
Nadhani kweli tunahitaji mabadiliko.......

emu-three said...

Naikumbuka hii nikifananisha kama vile polisi anayempiga kijana risasi eti kamtishia na manati ya ndege!

Mwanasosholojia said...

Huu ndio upuuzi wa mamlaka za dola nchini kwetu...maandamano ya amani, kwa nini yatawanywe kwa mabomu ya machozi...hivi, kama wangesindikizwa mpaka wanalikotaka kwenda (kwa Mkuu wa Wilaya), akawapokea na kuwasikiliza na kuahidi kuyafanyia kazi madai yao, na hata kuwatafutia usafiri wa kurudi shuleni, nini kingeharibika?Wakati sasa umefika kwa viongozi na mamlaka zao Tanzania kujifunza na kuitekeleza demokrasia ya kweli...ina-bore!