Thursday, May 5, 2011

HIVI HARUSI "NDOA" NI NINI?

Mara nyingi nimekuwa nikijiuliza hivi harusi "ndoa" ni nini? je ni mavazi, mwonekano, usafiri, chakula, vinywaji, muziki, watu, au ni UPENDO WA DHATI WA WATU WAWILI WAPENDANAO? Ebu angalia picha hizi hapa chini na sema unavyofikiri wewe karibuni ndugu zanguni:-

Picha hii ya kwanza mnaona wanaharusi ni harusi rahisi kabisa unadhani unaweza kufahamu yupi ni bibi harusi na yupi ni bwana harusi. picha toka kwa kaka Mjengwa

Na picha ifuatayo ni harusi "ndoa" iliyofanyika Ijumaa iliyopita kati ya Prince William na Kate.

7 comments:

emu-three said...

Harusi kwa ufupi ni sherehe ya kuwapongeza wanandoa. Mkishaoana wanajamii hujumuika na wanadoa kusherehekea hiyo siku muhimu. Kwahiyo basi harusi itajumuisha yote, mavazi, sherehe, makulaji nk
Ndoa ni kile kiapo cha makubaliano kuwa mimi Maisha nimekubali kuolewa na Mafanikio kwa `kanuni' kadha wa kadha....au sio

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

harusi sherehe nini sijui, ni uchizi fulani tu

Rachel Siwa said...

Naungana na kaka emu-three,Muhimu wanandoa wakikubaliana na kupendana kwa shida na raha!!!!!!Harusi/Sherehe ni matokeo ya nafasi zenu kipesa/kiuwezo.

Muhimu kufanya uliwezalo, si kuona mwingine kafanya sherehe kubwa basi nawe utake hata kama hali hairusu.

Niwazo langu!.

Simon Kitururu said...

Ndoa nikiapo.
Harusi ni chochote kitakacho kukosti fedha chenye gharama hata kama ni juisi ya miwa kitakacho endana na ndoa!


Na vyote na hisi ni ushahisi akili za Binadamu sio nzuri sana au ni dhaifu kiaina FULANI ambayo ikichunguzwa labda inaweza kugundulika ni ya utaahira kinamna fulani!


Unafikiri Malaika wanafanya hizi ndude?

Ushawahi kuchunguza BINADAMU waliojitungia maana ya maisha kwa kuvumbua kitu kiitwacho NDOA ili maishani kuwena MAANA fulanifulani za kubuni wahangaikavyo na HARUSI halafu ukaacha kustukia UKICHAA kidooooogo katika HAYO?:-(


Nimewaza tu kwa Sauti!

Penina Simon said...

Ndoa ni muunganiko wa watu wawili (jinsia tofauti) waliokubaliana kuishi pamoja kwa kufuata sheria kidini na kiserikali. Haijalishi kama wamevaa vizuri au wana muziki au usafiri, isipokuwa hayo yote hayo yote huwepo kukamilisha ile furaha yao na kuonyesha hadharani uma kuwa wao ni mme na mke.

Unknown said...

Safi, nimejifunza tofauti ya ndoa na harusi

Unknown said...

Nemejifunza mengi hapa