Sunday, May 22, 2011

JUMAPILI NJEMA :- ACHA KULIA NDUGU,MAMA,BABA!!!

Mwimbo huu nimeusikiliza mara kadhaa na kila nikiusikiliza unaniliza kinamna hebu sikiliza na wewe na uniambie kama nawe unalizwa:-( na Jehova Niss Tunduma!!!!

JUMAPILI NJEMA KWA WOTE!!!

12 comments:

Mwanasosholojia said...

Shukrani Da'Yasinta, tumeingia Jumapili pamoja na wengine labda kuwa na wakati mgumu wakiusubiri utabiri wa rapture wa mchungaji Harold Camping..uwe na Jumapili njema pia!

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mathew Ahsante ni kweli tumeiona jumapili pamoja. Na hata jumapili ijayo tutaina tu kama tunayo imani ya kweli. Mie jumapili yangu inaishia kulihengu/kazini...Jumapili njema.

Mwanasosholojia said...

Ni kweli dada yangu...I see, kweli kuwajibika mpaka Jumapili, pole lakini hongera..ahsante kwa neno jipya la kingoni (nafikiri) kwangu "kulihengu" teh!teh! "lihengu" njema (sijui nimepatia?) :) lol...!

Mija Shija Sayi said...

Matatizo mengi yatupatayo mara nyingi yasingetupata kama tungekuwa tunapata mafundisho mazuri na chanya juu ya kuishi. Tangu tunazaliwa tunaambiwa maisha ni magumu, ndoa ni ngumu, kazi ni ngumu,n.k. Mafundisho haya ya ugumu wa kila kitu yanapojaa vichwani mwetu basi hubadili fikra zetu na kuanza kuangalia mambo kwa mtazamo wa ugumu, matokeo yake tunaanza kukosa kujiamini, kunafuatiwa na kuanza kuonewa na baada ya hapo unaanza kukubali kuonewa na ukishakubali kuonewa huna la zaidi ila kuanza kulia na ukikubali kulia ujue umekwisha.

Wandugu tunatakiwa tubadili mitazamo yetu, tusikubali kuyatizama maisha katika ugumu hata kama yanaelekea katika ugumu, because what tou see is what you get. Ondoa wazo la ugumu maishani mwako/mwangu na weka wazo la rahisi sana, na tutashangaa jinsi maisha yetu yatakavyokuwa ya mteremko.

Simon Kitururu said...

Jumapili njema kwako pia Mrembo Yasinta!

Simon Kitururu said...

@Mija: Natafakari filosofia hiyo uliyomwaga kijiweni! Kifupi imenigusa!:-(

Anonymous said...

Nikweli ukiusikiliza hu wimbo kuna ka kulialia fulani kanakupata. Kaka S.

Yasinta Ngonyani said...

Pia angalia matendo yake...unajua hapa duniani kila mtu huwa anajifikiria mwenyewe tu kuwa yeye/mimi ndio nina matatizo makubwa lakini akija kusikia/kuona ya mwingine kwa kweli...ina bidi kulialia... na kama alivyosema da´Mija! nukuu:- "Ondoa wazo la ugumu maishani mwako/mwangu na weka wazo la rahisi sana, na tutashangaa jinsi maisha yetu yatakavyokuwa ya mteremko." Nakubaliana nawe.

Anonymous said...

Dada zangu, Da,mija na D,Yasinta,kuna kitu kinaitwa mazingira ya pahali ulipo au unayoishi yanachangia sana hicho kinacho itwa ugumu wa maisha.najaribu kuangalia kwa undani swala la' kuambiwa'au' mafunzo mazuri'kupewa ili uweze kumudu maisha yako.kiukweli wote hupata mafunzo ama huambiwa juu ya maisha najinsi gani mtu unaweza kujijengea maisha yalio bora.maranyingi mafanikio ya mtu katika maisha huja kama ndoto japokuwa kwa kiasi fulani ndoto ile uliitengeneza kwa njia moja ama nyingine.kwahiyo waweza kuambiwa, ukafundishwa lakini ukajikuta umefukuzwa kazi,au mkeo kakuacha.ugumu wa maisha kwetu sisi binaadamu nimoja katika mikimikiki yakuwapo kwetu katika dunia hii,na kama kielelezo cha binadamu kuyakabili maisha yake na mazingira yake kwa ujumla.wa weza kulia sana na kujilaumu na kujiapiza kwa tukio lililo kukuta nakusahau kuwa tukio hilo halikuja kwa bahati mbaya nimoja katika matukio kadha wakadha ambayo yaweza kumtokea binaadamu yeyete,la muhimu ni kukubali matokeo nakujifunza kitu kutokana na tukio hilo.unapozaliwa na kukua mengi unayasikia nakuyapitia lakini mwisho wayote hayo ni uelewa wako, na ufahamu wako katika kila jambo ulilo lifanya au kulisikia,iwe kwa kufundishwa ama kuambiwa tu,na ndipo tunapo ambiwa kila mtu na bahati yake.mfano,raisi obama wa marekani,ukimwangalia nakufuatilia jinsi maisha yake yalivyo kuwa,utagundua ,jinsi alivyo kuwa tayari kupambana nahali halisi ya mazingira aliyo kuwa akiishi,kakutana na vipingamizi vingi tu,mara alipo amua kugombea uraisi,lakini hakukatishwa tamaa,alijuwa ilikuwa ni kazi ngumu lakini ,nia jitihada ilikuwepo na dhamira pamoja na kuthubutu vilimfikisha hapo alipo sasa hivi kama raisi. Kaka S.

emu-three said...

Kweli dada yetu unatia simanzi kweli...!namshukuru kaka S kahitimisha kila kitu!

Rafikio Kay said...

Kwa kweli Yasinta nimesikiliza huu mwimbo nimejikuta natoa machozi ukizingatia kipindi ninachopitia kwa sasa.

Raymond Mkandawile said...

Ujumbe mzuri sana dada YAsinta japo nimechelewa kupitia siku ya jumapili lakini nimebarikiwa sana na ujmbe wa wimbo huu....Amen