Monday, May 2, 2011

NIFANYE NINI ILI MUME WANGU AWE NA HAMU NAMI?

Mume wangu anasema ananipenda sana, nami nampenda sana. Tuna watoto wawili wa kiume. Nimejaribu kila kitu cha kumfurahisha, kama vile kuvaa vizuri, kuandaa chakula kizuri akipendacho na kinywaji lakini Lakini mwenzangu haonekani kuridhishwa na jitihada zangu.
Baada ya chakula cha usiku huwa tunakaa na kuangalia Luninga huku tukiwa na vinywaji. Lakini cha ajabu nikimsogelea na kutaka niwe karibu naye ananiepuka. Yaani HATAKI hata nimguse ni kama NINANUKA au ninamsumbua vile.
Je, tatizo ni nini hasa, Je nanuka? Najiuliza na jibu sipati….Alimalizia kusema huyu mama huko chozi likimdondoka…......
Naam mara nyingi hivyo ndivyo inavyokuwa kwa sisi wanawake pale tukutanapo, si jambo geni sana kwa sisi wanawake kushirikiana kihisia. Ni jambo la kawaida kabisa kukuta mwanamke akimsimulia shoga yake anayemuamini juu ya madhila yake. Yote hiyo ni katika kutafuta nafuu na kuondokana na msongo wa mawazo.
Mara nyingi simulizi nyingi zinazowakutanisha wanawake ni zile zinazohusiana na mambo ya Ndoa, mahusiano, watoto au mambo ya kifamilia kwa ujumla, mara nyingi tunatamani kupata mahali pa kulinganishia, ili kutaka kujua kama tatizo nililo nalo lina ukubwa kiasi gani.
Ni hivi majuzi nikiwa kazini na mfanyakazi mwenzangu ndipo aliponieleza kile kinachomsibu kwa muda mrefu sasa, inavyoonekana, ni jambo ambalo alikaa nalo muda mrefu akijaribu kupambana nalo kimya kimya huku likiendelea kumtafuna, dada huyu wa Kiswidish.
Ili kujiridhisha na kutaka kujua ukweli halisi nikamuuliza kama amemuuliza mume wake jambo hili akajibu amefanya hivyo na jawabu alilolipata ni kwamba, mume wake huwa anachoka. Yaani kazi zake ni nyingi pia malezi ya watoto yanamchosha. Nikamuuliza kama hawawezi wakati wa wikiendi watoke ili kuwa peke yao? Hapo nikapata jibu ambalo sikutegemea. Alidai kwamba akisema hivyo mume wake anaona kama yeye anaamua nini wafanye.
Huyu mama akaendelea kusema, mimi ni binadamu Yasinta.,,,,,,,,,, Na nahitaji tendo la ndoa na sitaki kutoka nje kwani nampenda sana mume wangu. Nami sikuachia hapo kama mnavyonifahamu na u-Kapulya wangu nikamuuliza kama tatizo hilo lina muda gani au limeanza siku za karibuni?
Mama yule akashusha pumzi, akaniangalia kwa jicho la huzuni, kisha akajibu kuwa inatokea wanafanya tendo la ndoa mara moja kwa mwezi na hapo ni ile ya haraka haraka na halafu baada ya hapo mume wake anampa mgongo na kulala .
Hapo….akasita kidogo …nikamuuliza ulitaka kusema nini? Akaendelea unajua Yasinta mwanamke anahitaji kuandaliwa kwanza, mimi huwa siandaliwi kabisa........ Mweh! Nikaona makubwa haya ......nilikosa Jawabu la kumpa kwa kweli, nikabaki kuguna tu.
Hata hivyo nilijaribu kumshauri aende kwa washauri nasaha wa masuala ya Ndoa na mahusiano, lakini akadai kuwa mumewe ni mkaidi na hawezi kukubali.
Mwenzenu swala hili limenishinda maana sijui nimsaidieje! Je Wewe kama msomaji unaweza kunisaidia ni ushauri gani nimpe mama huyu, ili awe na furaha katika Maisha ya ndoa yake?
Ushauri tafadhali...........

14 comments:

Christian Sikapundwa said...

'KENGELAI'Dada Yasinta msaidie huyo mama ukweli anaumia kisaikolojia unajua tendo la ndoa si kuzaa tu watoto,bali nikufurahia tendo lenyewe ikiwa wote mkiwa katika mood ya kulifanya.

Sasa yanayomtokea huyo mama huenda anasababisha yeye kwa mmewe,hasa lungha kama si lugha ya wapendanao.'yule unasema nae ninani?,sikuhizi nakuona nae kila wakati ni bibi yako sio!'kila kukicha hakuna kulala unadhani bwana atakuwa na hamu.

Au kapata nyumba ndogo ambako anatimiziwa kisawasawa akifika kwake hana hamu.

Sasa mpe somo huyo,ajitahidi kumtafutia vitu ambavyo mme wake anavipenda,amwandalie,awe na lugha ya kumfanya kama alivyo mpata mara ya kwanza.wakiwa wawili avae mavazi ambayo yatamsisimua,kisha wakati anaona karibu anafanikiwa,yeye amwandae mmewe,atumie ufundi wake wakumfanya jamaa asahau matatizo yote.

Maandalizi ni kwa pande zote mbili si kwa bwana tu,hata kwa mke awe anajituma lakini ya kusema fanya tu ukichoka funika unafikili atampata,ataambulia mgongo tu.

Aidha amsaidie mmewe anasumbuliwa na saikolojia,wasiwasi na msongo wa mawazo hasa kwenye tendo la ndoa.Hasa kama amegundua kasoro katika mwili wa mkewe.Kazi kwako.(Na chilau mewawa)

Koero Mkundi said...

Kaka Christian nakubaliana na wewe lakini kama nimeelewa vizuri kutokana na maelezo ya huyo mama, ni kwamba amejitahidi sana kuihuisha ndoa yake,

Jamani keshasema anaandaa chakula kizuri, anajiremba na kumuandalia vinywaji murua ili kumshawishi mumewe awe na hamu naye lakini limjamaa limekomaa tu kuangalia Luninga na kisha kulala..
na kama likitaka kukata kiu ya (samahani ashakum si matusi) NYEGE zake anapiga za kichina china kisha anamgeuzia mgongo na kujilalia zake.....
Je ulitaka afanye nini zaidi ya hayo?

Kama ni mie wallahi wala nisingekonda, ya nini! Ebo! najitafutia King'asti changu na hapo ngoma inakuwa droo, akinigeuzia mgongo, mie akha, najua pumziko langu liko wapi, ya nini kukondeshwa na mtoto wa mwingine, kazaliwa peke yake na mie nimezaliwa peke yangu. sana sana tumekutana ukubwani...... Aaaaaaah! aende zake huko, asiniletee mie.....

Da Yasinta, mbinu moja ya kumshawishi na ambayo itamchoma roho huyo mwanamume aliyekufa GANZI ya mapenzi ni kwa huyo mwanamke kuanza kumpuuza na kufanya mambo yake bila kujali uwepo wake..... akijifanya yuko bize na yeye ajifanye yuko bize na mambo yake.... ipo siku tu atajiuliza kulikoni, mbona sibembelezwi kama zamani?

Unajua kawaida ya mijidume yenye silka hiyo ni kupenda utegemezi, yenyewe inataka kupendwa tuuu na kunyenyekewa, lakini wao Aaaaah! haiwahusu. Amchunie tu, nakwambia ni ndani ya wiki moja tu ataanza kujipendekeza.

Mapenzi ni kati ya pande mbili ukipokea ujue na kutoa, sasa mwenzetu yeye anapokea tuuu, lakini hata robo hatoi!

SIMON KITURURU said...

Sijui kwanini kauli nanukuu:``Huyu mama akaendelea kusema, mimi ni binadamu Yasinta.,,,,,,,,,, Na nahitaji tendo la ndoa ....´´´- mwisho wa nukuu.

.. Hiyo ndude imenifanya niwafikirie MASISTA na MAPADRE wa kanisa Katoliki ambao nasikia wanadunda shwari tu bila tendo la ndoa!


Kiharaka haraka kutokana na maringo yangu mwenyewe kama Mwanaume!

Majibu ya huyo Kidume ya kuhusu maswala ya Kazi na kulea kumfanyavyo achoke. Inaweza kuwa asemacho ni kuwa anamsongo wa mawazo utokanao na kuwaza familia kitu ambacho nafikiri ni code ya kuwa kifedha hayuko mahali pazuri na hilo kwake ni jambo la muhimu kwake.

Na kumbuka kama mgonjwa wako anaumwa tumbo labda sio tiba kujaribu kumtibu maumivu ya tumbo kwa dawa za fangasi za miguu. Dawa inatakiwa ishabihiane na ugonjwa kama nia ni kutibu ugonjwa.

Na kwa hilo nachojaribu kusema ni kuwa huyo mdada anaonyesha kujaribu kutibu ugonjwa kwa kutumia dawa isiyo ya ugonjwa. Mumeo anamsongo wa mawazo jaribu kuelewa ni nini hasa kinamsongoa wazo na sio kurupushani.

Tuko wengi mimi nikiwa mmoja wapo -kama niko nervous na kitu hata kuguswa sipendi naona usumbufu na sikawii kulala kwenye sofa badala ya kwenda pembeni ya kimwana nusu uchi chumbani kwa kuwa mchezo wa ndoa ni mchezo wa UBONGO. Wasichana kumbukeni kuwa ni ubongo utumao damu kwenye sehemu za siri ili Hamisi mdogo asimame kwa upande wa mwanaume. Na kama UBONGO unakabiliwa na jambo jingine kirahisi uume aka Khamis MDOGO anaweza asisimame kitu ambacho kinaweza kufanya shughuli nzima ya tendo la kupekechana liwe na dosari kimiingiliano sehemusehemu.

Kwa hiyo kifupi:
Huyu dada nafikiri anatakiwa kustukia tatizo hasa kabla hajaanza kuhangaikia tibabu.

Na tibabu inawezekana ni kumsikiliza mume na kujua kisawasawa kwanini yuko stressed na kulea na pia kazi kinamna hiyo. Na siri ya mahusiano shwari ni kuelewa mwenzio yuko wapi. Pili akumbuke kwa kuonekana kama anajajali sana tendo kuliko kitu kingine inaweza kuwa turn off kwa mwingine ambaye anahisi kuna jambo jingine muhimu zaidi linarukwa hata katika usikilizwaji.

Na kutokana na kauli zake za kujiuliza sijui ananuka! Labda hanuki ila kimuonekano havutii tena na siri ya kuvutia moja kubwa ni kujiamini- na kauli yake ya kujiuliza kama ananuka ni sign labda ya kuwa hajiamini kitu kifanyacho ana compasate mahali labda kwa kujaribu sana kitu - matokeo yake unajua kuwa kujaribu sana na maromansi ushabihiano wake ni mdogo sana.

Nimewaza tu kwa sauti na KUACHA!

emu-three said...

`Tendo la ndoa'...nimelianza hili makusudi, nikijiuliza moyoni ni kwanini hili likaitwa tendo la ndoa. Kupika kufagia, kufua kuosha vyombo, ukiwa unvifanya hivi ndani ya ndoa,haviitwi vitendo vya ndoa!
Kabla ya kuoana, wenzetu wazee waliotangulia waliandaa mambo mengi kwa watarajiwa wao, ikiwemo kufundana, kumfunda binti yao, ili ajue majukumu ya ndoa...
Kwanini walikuwa wanafanya haya. Kwasababu ndoa ni sehemu nyeti inayostahili mambo yake, na jambo muhimu ni hilo tendo la ndoa, ...hili waliliona kuwa `mtaalamu mzuri ni mwanamke..kama ilivyo katika kupika nk.(ndio hata wanaume pia wamo, lakini mpendezaji mkubwa katika tendo hili ni mwanamke),Na kama mwanamke hakujibidisha kwa hili, kwanza kwa kumvutia mumewe, pili hata kumfunza mumewe, itaishia `pabaya' swali je kama mwanaume ni mbumbumbu, haelekesi...tufanyeje?
Yupo jamaa kaoa karibuni, anasema mke wake ni mithili ya gogo, yeye akitaka kula chakula cha usiku analigeuza huku na kuhangaika huku na kule, huku mwenzake kalala, au kauchuna, eti anaona aibu akifanya vyakufanya ataonekana malaya, sijui...nikawaza sana nakujiuliza moyoni, ina maana huyu `hakufundwa' mbona kuna kitchen party, na alifanyiwa,...ilikuwa ya nini ile au ilikuwa ni sehemu ya burudani tu.
Ngoja nisiseme sana nitoe ushauri wangu mfupi kuwa `mwanamke mwema ni yule anayeijenga ndoa yake kwa kuwa mbunifu ...halikadhalika mmwanaume mwema ni yule anayejua kuwajibika ndani ya ndoa yake...na wavunjaji wa hili ni wanadoa wenyewe. Itakuwa ni makosa sana tukikimbilia kulaumiana, kwani haya majambo pia yanahitaji shule, yanahitaji busara, ...wewe kama mke wewe kama mume umeona hilo lipo ndani ya familia yako, tumie busara, soma, halafu kaeni chini jadilini, na ikishindikana tumia vishawishi na siku hizi kuna kanda zinafundisha vizuri kabisa, ikishindika wahusisheni wataalamu, au watu wa dini ili mpate tulizo la akili
...ndio maana nikatanguliza yale maneno `tendo la ndoa'
Tendo hili ni muhimu sana katika ndoa, tulisilidharau! Kwani ni tulizo la akili, ni sehemu kubwa sana katika ndoa zetu. Jengeni ndoa zenu kwa kuambizana, kushauriana na sio kuonyeshana ubabe!

Goodman Manyanya Phiri said...

Amri ya kwanza kutoka kwa Mungu ni kwamba tuzae na tuwe wengi duniani.


Kama ni hivyo, si lazima tuzae na waume zetu.Inamaana: silazima tufanye mapenzi nao!

Mwanasosholojia said...

Mmmh, hapa...mmmh, tatizo si kama unavyoweza kulifikiria kwa haraka..ni zito na linalohitaji umahiri kweli kulitolea ushauri...ngoja kwanza niendelee kupekecha kichwa

tanzaniasports.com said...

Mpe contacts zetu.......

Salehe Msanda said...

Habari,
Nadhani inabidi huyo dada amepe nafasi mume wake na kumvumilia kidogo,wataalamu wa masuala ya mahusiana na ndoa wanasema kuna wakati huwa inatokea wawili mmoja wao kutokuwa na hamu na mwezake kutokana na sababu mbalimbali,wanasema kama sikosee kuna kuingia pangoni kwa mwanamke au mwanaume(sina uhakika sana) nitajaribu kuingia katika maktaba yangu na kukueleza kilichoandikwa.

Inapotokea hali kama hiyo inabidi kila mmoja amumpe nafasi mwenzake na ndiyo maana enzi hizo babu zetu walikuwa wanawasafirisha wenza wao wanakaa mbali na wao ili kuruhusu kipindi hicho kupita. Then kunahali ya kutaka kuwa karibu baina yao hujirudia.

Jaribu kutembelea tovoti ya utambuzi kuna swali kama hilo liliiulizwa na shaban kaluse na kutolewa maelezo.
Kila la kheri.
kazi njema

Penina Simon said...

Nimejiuliza ni kwa nini hutokea hivyo, Nikaona kama Yasinta haukutufafanulia vizuri hapa.
Wakati mwingine hutokea hivyo, kutokana na jinsi walivyooana, labda walikutana muda mfupi wakahisi wanapendana, au walishinikizwa na ndugu,marafiki,au hali fulani, sasa wakikaa baada ya muda mmoja akaanza kujuta, na hiyo ndoa daima haiwezi kuwa na amani, labda mwanamke huyo adumu kusugua magoti na kumwomba mungu vinginevyo hata angeweka vionjo gani hapana asubuhi kwao.

Kabinti said...

Habarini,
Nimeona hiyo post nikaumia sana kwa sababu na mimi nina shida kama hiyo.
me mume wangu hata ikitokea nikamfuata akafanya uume wake unasimama ila sio sana, unakuwa bado umelegea.
nampenda sana mume wangu na siwezi kutoka nje.
Hiyo ilipelekea nikapeluzi sana ili kujua tatizo.
tunaishi hivyo ni zaidi ya mwaka, na mara zote me ndo huwa namfuata. yeye hawezi kunitamani.

kitu ambacho nimegundua ni kwamba huwa inatokea mwanaume anakuwa hana hamu bila kuwa na tatizo lolote.
Kuna wakati inabidi kujitoa mambo ambayo hatupendi kwa ajili ya wapenzi wetu.

Wapendwa tusaidiane ushauri.

Ferdinand Mlandali said...

Ndugu zanguni!
Hapa hapana mchawi na tusitafute mchawi ila tutambue kuwa ndoa ni mpango wa Mungu ili watu waishi pamoja kwa amani, upendo na kufurahiana wawapo pamoja au hata km hwapo pamoja kwa wakati huo. Lazima tutambue kuwa anayepiga vita watu kufurahiana ni shetani na anatamani watu waishi kwa majozi kila iitwapo leo. watu wanachangia eti naye angemtafuta mtu nje ya ndoa yake ambaye atamfurahisha na kumridhisha. Baada ya hapo what next? Huko kote ni kujisumbuatu. Suluhisho kamili la tatizo hili ni kumwamini na kumwomba MUNGU aingilie kati kwani ndiye ajuae chanzo cha tatizo.
Asanteni

Japhet Kamkono said...

Heee!mwee!
Tatizo katika tendo kuna mambo kadhaa ambayo yanasababisha:-

1.Kutokua na mawasiliano.Kila MTU anaishi kama vile yuko gheto.Mwanamme amejikita kutafuta ili alishe familia na mwanamke umejikita kucheza na wanao au mwanao na kumpuuza mumeo.

2.Mwanamke kua mpumbavu.Mumeo amesota kutwa nzima kwenye mihangaiko anarudi nyumbani hakuna kumpokea,kumfariji,kujua kazini kulikuaje hamna.Unacho jua wewe mwanamke ni kumwambia "mbona haukuacha hela ya sukari,mbona uliondoka haukuacha kitafunwa".Hapo mwanaume anaye wajibika umemchefua sana hata kama utajipendekeza ili mt**me.Hawezi kabisaaa tena ukizidisha anakugonga makofi.

3.Mwanamke wewe ni mvivu sana.Tena boya la kufikiri haujui maisha jinsi yalivyo.Jaribu kubuni kitu cha kufanya uona mwanaume wako atakavyokupenda.Sio pesa ya kuhongwa na hawala yako hapana.Fanya jambo dogo sana ambalo ataliona mumeo halafu kupitia jambo hilo msaidie mahitaji ya ndani.Nunua sabuni,sukari,chumvu,unga Wa ngano na nk.Utaona jinsi atakavyo kufungulia moyo na kuanza kukuhadithia mkwamo Wa kipesa alionao pamoja na matatizo kazini kwake.

4.Usimuombe pesa ya kijinga wakati amejituliza pekeyake.Muache siku akifurahi ukaona anacheza na watoto wenu kama mnao ndo uombe.Pesa ya kijinga kusuka,mchezo,kununua kwa chinga anaye pita mtaani pako,kufua na kupasi nguo kwa dobi.Kwa mwanaume mwenye msongo Wa mawazo hayo yote ni ujinga.

5.Wewe naye mwanamke ni kero sana kwa mumeo toka mmeoana kila akitaka avue zake halafu wewe kuvua walaaa!Mpaka aanze kusumbuka kama vile anakubaka huo ni ujinga mshukuru Mungu nakupa ushauri Wa bule na Shukuru mumeo ni mwaminifu angekutimua zamani.Mkianza kut**na wewe ulivyo lala ndo hivyo hivyo unakera sanaa tu.Ndio maana mwanaume wako hana mpango na hapo amekutega sana danganyika ukatom**she nje itakua ndio sababu yakukurudisha mkoani kwenu.

6.Unajaribu kusoma hisia za mume wako hauwezi hauwezi kamwee!Mwanamume anataka uwazi sio usome hisia zake.Vitendo vyako vya kutwa nzima vimemboa sana halafu wewe ikidika usiku unajinyeg**sha ili mti**ne.Haiwezekani kabisaa.Chakufanya anza kumwambia.

7.Kila wenza wanamaneno yao na muziki wao ambao hutumia kutaarifiana iwapo wanahitajiana.Mwambie kabisaa baba katatii mchana utarudi...uwahi utakuta chakula ...taja alichokua anakipenda enzi zile.Andaa hichohicho kisha mwambie nitakupikia na k**ma uje umejiandaa.Utasikia anajifaragua aaaa umeanza..wanawake bwana mnawaza hayohayo.Wenzenu wana waza maendeleo ninyi....basi hapoutakua umempata.

UKIMKOSA HAPO Tunaanza maombi atakua amependwa na jini mahaba na litakua linampa K**ma ya kijini ndotoni na wewe utakua unaota mumeo anamwanamke.Lengo la jini huyo ni kuachanisha ndoa yenu.Niandikie kwa nia njema nikushauri na tuombe pamoja.Kamwe usimpeleke mumeo kwenye baràza la masuala ya ndoa ukimpeleka huko umevunja mji wako mwenyewe.
0786249030

Madiko said...

Mume wangu anampendelea mke mkubwa wakati mm namfanyia kila kitu kinapenzi kupendeza utaratibu ila mumewangu ataki kulala kwangu mke mkubwa anamtukana ajamzali mwaka wasaba mm ninamimba ameniowa yapata mwaka na uja akinishtakia maudhi ya mkewe nahataki mkewe ajue ameowa ila amenijulisha kwa wazazi wake nanimependwa ila mke wakwanza hatakiwi sielewi haswa anampendea nn ata tendo la ndoa amridhishi ananielezea kila kitu mm ananitimizia ila kwangu akija anajiiba awezi kulala na anamuogopa mke mkubwa kupita maelezo mm nimdogo mkewake nimkubwangu sana na zaidi anamtukana mume sana hadi mzazi wa mume anaomba mume wangu amuache ila mume anashindwa kumuacha sielewi naomba munieleweshe nachanganyikiwa

ray njau said...

KIFUNGO CHA NDOA KINAPOKUWA HATARINI
.........................................
Wale wanaoumia moyoni kwa sababu ya uhusiano wao wa ndoa labda wanajiuliza hivi: ‘Je, ndoa yangu isiyo na furaha inastahili kweli kuokolewa? Laiti ningeweza kuanza maisha mapya na mwenzi mwingine wa ndoa!’ Huenda wakaanza kufikiria kuvunja kifungo chao cha ndoa wakijiambia hivi: ‘Ooh, ninataka kuwa huru tena! Kwa nini nisimtaliki? Hata kama siwezi kupata talaka ya Kimaandiko, mbona tusitengane ili nifurahie maisha tena?’ Badala ya kufikiri kwa njia hiyo au kuwazia jinsi ambavyo mambo yangekuwa, Wakristo wanapaswa kujitahidi kuboresha hali yao ya sasa kwa kutafuta mwongozo wa Mungu na kuufuata.
Ikiwa Mkristo atapata talaka, huenda awe au asiwe huru kuoa au kuolewa tena kwa msingi wa Kimaandiko. Yesu alisema hivi: “Mtu yeyote anayemtaliki mke wake na kumwoa mwingine, ila kwa sababu ya uasherati, anafanya uzinzi.” (Mt. 19:9) Katika andiko hilo, neno “uasherati” linatia ndani uzinzi na dhambi nyingine nzito zinazohusiana na ngono. Ni muhimu Mkristo asali na kutafakari kwa uzito ikiwa anafikiria kumtaliki mwenzi wake wakati ambapo hakuna yeyote kati yao aliye na hatia ya kufanya uasherati.
Ndoa inapovunjika inaweza kuonyesha kwamba hali ya kiroho ya mtu imedhoofika. Mtume Paulo aliuliza swali hili zito: “Kwa kweli ikiwa mtu yeyote hajui jinsi ya kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje kutaniko la Mungu?” (1 Tim. 3:5) Kwa kweli, wenzi wote wawili wanapodai kuwa Wakristo na bado ndoa yao inavunjika, huenda watazamaji wakafikiri kwamba kwa kweli watu hao hawatendi kupatana na mambo wanayohubiri.—Rom. 2:21-24.
Wenzi wa ndoa waliobatizwa wanapopanga kutengana au kutalikiana kwa msingi usio wa Kimaandiko, bila shaka wana tatizo la kiroho katika maisha yao. Ni wazi kwamba mmoja wao au labda wote wawili hawafuati kanuni za Kimaandiko. Ikiwa kweli walikuwa ‘wakimtegemea Yehova kwa moyo wao wote,’ hakungekuwa na sababu yoyote ya kuamini kwamba wangeshindwa kuizuia ndoa yao isivunjike.—Soma Methali 3:5, 6.
Ndoa nyingi ambazo zilikuwa zinaelekea kuvunjika, baada ya muda zimefanikiwa sana. Wakristo ambao wanaazimia kutovunja haraka-haraka ndoa yenye matatizo mara nyingi wanapata thawabu kubwa. Fikiria jambo linaloweza kutokea katika familia iliyogawanyika kidini. Mtume Petro aliandika hivi: “Ninyi wake, jitiisheni kwa waume zenu wenyewe, ili, ikiwa wowote si watiifu kwa lile neno, wavutwe bila neno kupitia mwenendo wa wake zao, kwa sababu wamekwisha kushuhudia kwa macho mwenendo wenu ulio safi kiadili pamoja na heshima kubwa.” (1 Pet. 3:1, 2) Naam, mwenzi ambaye si mwamini anaweza kukubali kweli kwa sababu ya mwenendo mzuri wa mwenzi wake mwamini! Ndoa hiyo ambayo imeokolewa inamletea Mungu heshima na inaweza kumletea baraka nyingi mume, mke, na watoto ambao huenda wakawa nao.
10 Wakristo wengi waseja wanachagua waamini wenzao waliojiweka wakfu kuwa wenzi wa ndoa kwa sababu wanatamani kumpendeza Yehova. Hata hivyo, hali zinaweza kubadilika kwa ghafla. Kwa mfano, katika visa fulani, huenda mwenzi wa ndoa akapata matatizo makubwa ya kihisia. Au muda mfupi baada ya arusi, huenda mwenzi wa ndoa akawa mhubiri asiyetenda. Kwa mfano, Linda,* Mkristo mwenye bidii na mama mwenye upendo, alitazama bila kujua afanye nini mume wake aliyebatizwa alipoanza kujiendesha kwa njia isiyopatana na Maandiko bila kutubu, na hivyo akatengwa na ushirika. Mkristo anapaswa kufanya nini ikiwa inaonekana kwamba ndoa yake imeharibika kwa sababu kama hiyo na hakuna matumaini yoyote?
Huenda ukajiuliza hivi: ‘Je, ni lazima niendelee kujaribu kuiokoa ndoa yangu hata hali ziweje?’ Hakuna mtu anayeweza au anayepaswa kukufanyia uamuzi huo. Hata hivyo, kuna sababu nzuri za kuendelea kuimarisha kifungo cha ndoa kinachodhoofika bila kukata tamaa. Mungu anamthamini sana mwanamume au mwanamke anayemwogopa ambaye anavumilia majaribu katika ndoa yenye matatizo kwa sababu ya dhamiri yake. (Soma 1 Petro 2:19, 20.) Kupitia Neno lake na roho yake, Yehova atamsaidia Mkristo ambaye anajitahidi kabisa kuiimarisha ndoa yake yenye matatizo.(www.jw.org/sw)