Sunday, May 15, 2011

TAFAKARI YA JUMAPILI YA LEO!!

Wakati mwingine tunaweza kuyaona maisha hayana maana/hakuna haja ya kuishi. Lakini hakuna Mungu ambaye kila wakati yupo kwa kubadili hali hiyo. Tusipoteze imani/tumaini yetu/letu kwa Mungu. Kwani mwisho atakuja kubadili hiyo hali. Hata kama mti uliukata kuna tumaini/imani siku moja utaota tena. TUKUTANE TENA JUMAPILI IJAYO ......MPAKA HAPO MWENYEZI MUNGU AWE NANYI NA ATAWALE NYUMBANI WENU/MWAKO DAIMA.....!!!!!

Muda si muda nikapita hapa na kukuta habari hii nikavutiwa nayo hebu nawe fungua hapa ufaidi. Tujifunze Kusini . Ahsante sana kwa hili.

11 comments:

Simon Kitururu said...

Mmmh!

Yasinta Ngonyani said...

Mmmh! nini tena Mtakatifu?

Simon Kitururu said...

Mmmmmmmmmmmmh!

Yasinta Ngonyani said...

Haya bwana nakutakia na wewe j2 njema pamoja na miguno yako hata kama sielewi maana yake ni nini?

Simon Kitururu said...

@Nangonyani: Ni tafakari tu za Jumapili mtu wangu na kwakuwa posti yako imeegemea katika IMANI za dini fulani,...
...
sa nyingine kuguna ni sentensi nzuri kuliko kusema nachofikiria ambacho kwa wenye imani hawawezi kuelewa hasa kwa kuwa kama mtu ana imani huo ni ushahidi kuna mambo hatumii akili kutatua. Kwa kuwa IMANI na kutumia akili ili vitu vi ``MAKE SENSE ´´ labda hakuna uhusiano mzuri!:-(


Mmmmmh!:-(

Yasinta Ngonyani said...

Sasa naona tupo pamoja, Ahsante sana kwa kufafafanua hiyo Mmmhh! yako.:-)

chib said...

Jumapili njema na kwako pia

Mzee wa Changamoto said...

Duh!!

Unknown said...

Najaribu nami kujihudhurisha katika mjadala wa maoni kuhusu tafakari la leo.
POST YANGU ITAKUWA NDEFU KWA SABABU YA USONGO WA KUTOPOST HAPA.

Yesu alikuwa Myahudi mwanamume aliyeishi miaka 2000 hivi iliyopita (labda 6 KK - 30 B.K.). Kutokana na umuhimu wake katika historia ya binadamu, kwa kawaida miaka yote inahesabiwa kwanzia ujio wake (ulivyokadiriwa kimakosa katika karne ya 6).

Mazingira yake
Nchi ambayo Yesu alizaliwa akafundisha ni nchi ileile ambayo Mungu aliwaahidia Waisraeli tangu zamani za Abrahamu, ni nchi ileile waliyoiteka chini ya Yoshua, ni nchi ileile waliyoirudia kutoka utumwani Babeli.

Lakini wakati wote wa Agano Jipya, yaani tangu Yesu alipozaliwa hadi mwisho wa maisha ya mitume wake, nchi hiyo haikuwa huru, bali chini ya himaya ya Warumi, ingawa pengine hao waliwakabidhi vibaraka, yaani watawala wenyeji waliowekwa na wakoloni.

Vibaraka hao ni Herode Mkuu (37 KK-4 KK) na wazawa wake, ambao tena hawakuwa Waisraeli halisi bali Waedomu ingawa kabila lao lililazimishwa kuingia dini ya Kiyahudi karne iliyotangulia. Ukoo huo unajulikana kwa ukatili, uchu wa madaraka na uzinifu wake.
Vilevile maliwali wa Kirumi waliowekwa pengine kutawala nchi au sehemu fulani walionyesha mara nyingi ukatili na dharau kwa Waisraeli na dini yao, hata kusababisha chuki na mapigano kati ya jeshi na wananchi. Mfano mmojawapo ni Ponsyo Pilato aliyesimamia Uyahudi kuanzia mwaka 26 hadi 36 B.K.
Mbali na hayo, utawala wa Roma, ulioenea Ulaya Magharibi na Kusini, Afrika Kaskazini na nchi za Mashariki ya Kati kupakana na Iraq ya leo, kwa jumla ulihakikisha hali ya amani kwa muda wote wa Agano Jipya na karne za kwanza za Kanisa. Hali hiyo, pamoja na umoja wa dola hilo lote, na urahisi wa mawasiliano kwa njia ya barabara zilizotengenezwa na Warumi, na uenezi wa lugha ya kimataifa (Kiyunani yaani Kigiriki cha zamani), ilichangia kasi ya uenezaji wa habari njema (Injili). Lugha hiyo ndiyo iliyotumiwa na waandishi wote wa Agano Jipya ili vitabu vyao viwafaidishe watu wengi zaidi, ingawa baadhi yao hawakuijua vizuri.
Lugha asili ya Yesu na ya Mitume ilikuwa Kiaramu ambacho ni jamii ya Kiyahudi na ambacho polepole kilishika nafasi yake kati ya Wayahudi kuanzia karne ya sita K.K. Hao wote walitokea mkoa wa Galilaya, uliokuwa na mchanganyiko wa watu (Waisraeli na mataifa), kiasi kwamba huko Wayahudi wenyewe walifuata kwa urahisi desturi za Kiyunani hata wakadharauliwa na wenzao wa Kusini (Yerusalemu na mkoa wa Yudea).
Kati ya mikoa hiyo miwili ulienea mkoa wa Samaria ambao wakazi wake walijenga uadui mkubwa na Wayahudi baada ya uhamisho wa Babeli, walipokataliwa kuchangia ujenzi wa hekalu la pili la Yerusalemu.

emu-three said...

Ujumbe murua, nadhani sijachelewa nawo!

Salehe Msanda said...

Habari

Somo lililopa katika habari ya jumapili ni kututaka tufahamu kuwa kila jambo linalotutokea linasehemu kuu mbili,sehemu ya uzuri wa jambo husika na sehemu tunaita ya machungu.

Tunachotakiwa kufanya ni kuchukua upande chanya wa jambo. Kitu ambaocho tulio wengi tunashindwa tu wepesi wa kuangalia upande unaoumiza kwa kila jambo linalotutokea.

Tuwe na tafsiri ya upande unatupa matumaini mbadala ya kutafsiri jambo kwa kujiumiza.

Wataalamu wa saikolojia wanasema kuliangalia jambo kwa uzuri au kila wakati kujaza mawazo yetu na kufikiri vizuri badala ya kufikiri vibaya. Inawezaekana pamoja na kuwa kutokana na mazingira tuliyokulia inaonekana kama kitu kisichowezekana kuwaza/kufikiri mambo mema kwa muda mwingi. Soma kitabu cha munga katika eneo la sisi ni nani. Kitabu cha maisha na mafanikio

J3 njema