Thursday, May 19, 2011

WAKATI HUU JOTO LIANZAPO UKIONA SIPATIKANA BASI UJUE NIPO MAENEO HAYA:-)

Anaandaa ili apande maua mengine...
Haya aliapenda mwaka jana na ameshapalilia ....

Hapa pia na sasa yameanza kuchanua chanua.....



Dada huyo hatosheki na maua tu.....


Hapa ni Rabarber au RHUBARB...unaweza kutengezeza kinywaji , pia kutengeneza pei "paj" ila sasa kinachoniuma ni kwamba haya majani ni mazuri mno kwa kutumia/kula ma mchicha vile:-(


Na ukinikosa sehemu hizo zoooote basi nitakuwa hapa kwenye terrace "altan" napumzika huku nikinywa chai yangu. Na pia kusoma chochote ambacho kitanifanya nipumzike angalao kwa dakika chache kuupumzisha "mgongo"....Kwa hiyo maua/bustani ni vitu ambavyo napenda sana ni "HOBBY" zangu......

11 comments:

John Mwaipopo said...

ni wakati wa kutafakari na kutafakuri yaliyopita na yaliyopo tayari kwa winter ijayo.

Anonymous said...

Ahhh hiyo safi sana Dada yasinta unajua jinsi ya ku spend time, pia ni fundisho kwa wanawake wengine kuwa kama wewe, kutunza mazingira yao wengi wao hata huku kwetu unakuta hata kuweka sawa ni shida kisa nyumba si yake na hata kama ni yake nyumba utakuta mazingira si salama.

Big up sana dada.



Ben
S/korea

EDNA said...

Waooh hongera mdada.

Mwanasosholojia said...

Imekaa vizuri sana hii Da'Yasinta

Salehe Msanda said...

Ok
Kila la kheri,maua ni sehemu mojawapo yakutufanye tutulie na kutafakari na kujipanga upya

Shughuli njema

Yasinta Ngonyani said...

Mta.Simon Si utani ni kweli kabisa...
Kaka John..Hakika umenena haswaaaa!

Ben wa S/Korea!
Ahsante kwa kutembelea hapa Maisha na mafanikio na karibu tena na tena. Pia ahsante kwa wasifu wako.

Edna! Ahsante sana na unakaribishwa kuja kunisaidia..LOL

Kaka Mathew! Ahsante sana kwa hilo...
Kaka Salehe! ni kweli kabisa na tena ikibidi unaweza kuongea na maua yako mie huwa nafanya...

Unknown said...

Sawa Bwana

chib said...

Ndio tofauti ya huko na huku

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mcharia! Haswa!

Kaka Chib! ni tofauti kubwa sana kwani hapa huu ndio wakati ambao sio kufurahia maua tu pia hata kuwaona majirani wanatoka nje....ajisikiaye vidole vinawasha anakaribishwa sana kuja kuchezea udongo:-)

Mija Shija Sayi said...

Yasinta nipo mbioni kuja kukutembelea...usiulize lini.

Yasinta Ngonyani said...

Mija KARIBU SANA...na wala sitauliza na siulizi lini kwani napenda sana ugeni wa kushtukia...:-)