Monday, February 3, 2014

MSAADA WA VITENDAWILI NA MAANA ZAKE!!

Nimetumiwa ujumbe huu lakini kwa bahati mbaya hivi vitandawili kwangu vimekuwa vigumu kidogo kwa hiyo naomba ndugu zangu tusaidiane maana palipona wengi hapaharibiki kitu..Natunguliza shukrani zangu za dhati kwenu. Na ujumbe wenyewe unasema hivi:- karibuni!!
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Dada Yasinta, habari za leo? Samahani naomba msaada wako kwa vitendawili vifuatavyo:
1) Wanastarehe darini.
2) Sina dada wala kaka, lakini baba wa huyu jamaa ni mtoto wa baba yangu.
3) Nguo ivaliwayo kila siku isiyoingiwa na chawa.
4) Ini la ng'ombe huliwa hata na walio mbali.
5) Chatembea na hakijapata kupumzika hata nukta moja.
6) Mvua kidogo ng'ombe kaoga kichwa.
7) Njoo hapa nije hapo.
8) Msitu ambao haulii hondohondo.
9) Aliwa, yuala, ala, aliwa.
10) Ajenga ingawa hana mikono.
JUMATATU IWE NJEMA KWA WOTE!

18 comments:

Anonymous said...

Da Yasinta. Shikamoo!

Haya hapa majibu.
1. Panya
2. Mtoto wangu
3. Nyusi
4. Kifo
5. Jua
6. Jiwe
7. Kiraka
8. Mimba
9. Papa
10. Ndege

By Salumu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Salumu ahsante sana kwa mchango wako..Hapi kwenye namba tano mimi nilikuwa na jibu ...Saa

Anonymous said...

Sasa da Yasinta usemapo saa, ni saa ipi? Ya kujaza na ufunguo au ya betri na hizo zote zinaweza kuharibika. Ki sayansi hata jua halitembei! Labda tuseme ardhi (dunia) ndio inazunguka jua na mwezi inazunguka dunia. Maajabu ya Mwenyezi Mungu haya! By Salumu.

NN Mhango said...

Pamoja na kuwa kipanga shuleni sikuyajua haya madude. Hivyo msaada wangu hapa ni kidogo au tuseme hakuna. Hata hivyo nashukuru nimepata mawili matatu na kuelimika.

Peter Moshi said...

Nakushukuru kwa kutuelimisha dada. Naomba msaada wa vitendawili hivi. ..1)Kiti nyikani,2) Kazi ni pantosha, 3) Kwetu tunalala tumesimama,4) Mama yupo chini ya wanawe wananing'iniquity darini, 5) Msichana wangu mrembo lakini havutiki,6)Ninakupa lakini mbona huachi kunidai, 7) Nakunywa mchuzi na nyama natupa nyama , 8) Ndege wengi baharini, 9) Teremka mlina kwa urahisi, 10) Tamu ya chumvi

Peter Moshi said...

Nakushukuru kwa kutuelimisha dada. Naomba msaada wa vitendawili hivi. ..1)Kiti nyikani,2) Kazi ni pantosha, 3) Kwetu tunalala tumesimama,4) Mama yupo chini ya wanawe wananing'iniquity darini, 5) Msichana wangu mrembo lakini havutiki,6)Ninakupa lakini mbona huachi kunidai, 7) Nakunywa mchuzi na nyama natupa nyama , 8) Ndege wengi baharini, 9) Teremka mlina kwa urahisi, 10) Tamu ya chumvi

JACKSON said...

Yaan vitendawili ni vigumu sana,,kuna swali hapa kwamba kutokana na mabadiko ya sayansi na teknolojia vitendawili havina maana jadili kwa kutumia vitendawili sita.

STELLA MURUNGI said...

Kiatu kisichoisha. .......?

caroline mbaabu said...

Tafadhali niambie jibu LA kitendawili hiki/- juma kalala na ndevu kaziacha nje
2. Ngozi ya babu chui inapedwa sana

Anonymous said...

Mimi pia naomba unisaidie na jibu la kitendawili iki agnes maridadi.

Unknown said...

ningependa msaada katika kujibu kitendawili kifuatacho.
wanatembelea lakini hawatembelewi

Unknown said...

Tafadhali unisaidie kitendawili hiki, watoto wa binadamu wa.......

zuwena kambi said...

Naomba majibu ya vitendawili hivi;
1.Hana adabu wala stash
2.Hausimiki hausimami
3.Ajenga ingawa hana mikono
4.Kila nikitembea nasikia wifi wifi
5.Fuu funua fuu funika

John Nyalusi said...

Msaada wa maana ya vitendawili.
1.Ukumbuu wa babu ni mrefu
2.Nichangu lakini sikitumii

Johad Joseph said...

Kitendawili-kila akija kwetu hutanguliza na kelele

Unknown said...

Naomba mnipe jibu la kitendawili hiki
Nyanya apepeta ufuta

Unknown said...

Naomba mnipe jibu la kitendawili hiki
Nyanya apepeta ufuta

Unknown said...

Bara bara

Jina