Monday, March 5, 2018

NI WIKI NYINGINE NA NI JUMATATU NAMI NIMEONA TUANZE HIVI.....

Nimekumbuka sana enzi zile ambapo tulikuwa tunakula chakula/vyakula kwa pamoja. Lakini  siku hizi umezuka mtindo wa watu kula chakula kila mtu sahani yake. JE? wewe  hii unakumbuka wapi?

4 comments:

Juma Mtwana said...

Huo ni ugali wa muhogo sio;

Yasinta Ngonyani said...

Kaka yangu Juma ahsante sana kwa kupita hapa kwetu kila mara ! mimi ningesema ni ugali wa ulezi...ah

ray njau said...

Hizi zama za simanzi(sayansi) na teke linalokujia(teknolajia) zimetuondolea uke ukaribu wa kifamilia kutoka enzi za wahenga.

Yasinta Ngonyani said...

haswa kaka Ray...hakuna kutembeleana tena wala kuandikiana barua...natamani siku zirudi nyuma